in

Chat kwa Namna ya Kipekee kwa Kutumia Njia Hizi (Android)

Hizi hapa apps nzuri zinazoweza kusaidia kuchat kwa namna ya kipekee

Chat kwa Namna ya Kipekee kwa Kutumia Njia Hizi (Android)

Ni wazi kuwa siku hizi watu wengi zaidi wamekuwa wakipendelea kuwasiliana kwa kuchat zaidi kuliko kupiga simu, hii imefanya app kama WhatsApp,Telegram na nyingine kama hizi kuwa na umaarufu mkubwa. Hii ni moja ya sababu ambayo imesababisha leo nikuletee app hizi nzuri ambazo unaweza kuzitumia kurahisisha zaidi mawasiliano yako hasa ya kuchati.

Kumbuka app hizi ni nzuri sana na zinapatikana kwenye soko la Play Store hivyo unaweza kudownload app hizo kwa kubofya link yenye jina husika baada ya maelezo ya app yenyewe. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie app hizi nzuri.

Kama ungependa kusoma meseji za WhatsApp bila kuonekana online, au kuangalia status bila kuonekana kama umeangalia status basi app hii ni nzuri sana kwako.

Kupitia app hii itaweza kusoma meseji za WhatsApp bila kuonekana online na pia ukituma meseji huwezi kuonekana online, app hii ni rahisi kutumia na inafanyakazi kwenye simu zenye mfumo wa Android kuanzia Android 5.0

Download App Hapa

Bluetooth Chat
Price: Free

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android na unapenda kuchati na ndugu jamaa au marafiki mkiwa karibu karibu au kama wewe ni mwanafunzi na ungependa kuchat na rafiki yako mkiwa kwenye darasa moja na lingine basi app hii ni nzuri sana kwako.

Apps (7) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2022)

App hii itakupa uwezo wa kuchat bila Internet na utaweza kutuma meseji pamoja na picha kwa kutumia Bluetooth, app hii ni nzuri sana kama unataka kutunza kiasi cha bando hasa pale mnapokuwa karibu karibu.

Download App Hapa

Kama unataka kutuma meseji ambazo zinakuwa na uwezo wa kujifuta zenyewe kwa wakati fulani basi wewe na marafiki zako mnahitaji app hii ya Mei.

App hii inatumia mfumo wa AI kuweza kufanya mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kupanga meseji zako kutokana na makundi na pia utaweza kuseti meseji kuweza kujituma kwa muda flani, pia meseji hiyo kufutika pale mtu atakapo maliza kusoma meseji hiyo. Kama unataka usalama na utaki meseji zako kusomwa mara mbili basi app hii ni nzuri sana kwako wewe na marafiki zako.

Download App Hapa

Daywise ni app nzuri ambayo itakusaidia kuweza kupata ujumbe kwa wakati ambapo hauko bize. Mara nyingi ukiwa kwenye kikao au ukiwa umelala ni lazima kuweka simu yako Silent, lakini app ya Daywise inaweza kusaidia kuweka silent kwenye upande wa meseji pekee na utaweza kupokea meseji wakati ambapo wewe umeseti tu.

Hizi Hapa Apps Nzuri za Android Kwaajili ya Wanafunzi

App hii ni nzuri kwani utakuwa na uwezo wa kupokea meseji lakini hutoweza kupata Notification hivyo baadae unapo pata muda utaweza kusoma meseji zako kwa urahisi.

Download App Hapa

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unataka kujifunza lugha mbalimbali na kama unataka kuchati na watu mbalimbali kutoka nchi mbalimbali wakati unajifunza basi download app hii ya HelloTalk.

App hii inakupa uwezo wa kuchati na watu ambao wanaongea lugha tofauti na app hii itakusaidia kubadilisha lugha na utaweza kujifunza lugha kwa urahisi. App hii ni nzuri sana na inavuti kuchati na watu kwenye app hii ijaribu sasa utaniambia.

Download App Hapa

Na hizo ndio apps nilizo kuandalia kwa siku ya leo kama unataka kujua apps nzuri zaidi unaweza kusoma hapa apps nzuri kwaajili ya wanafunzi. Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.