in

Series Ya Infinix Hot Kuja na Sifa Hizi Kwa Mara Ya Kwanza

Simu hii inatarajiwa kuwa na teknolojia ya kuongeza RAM hadi GB 7

Series Ya Infinix Hot Kuja na Sifa Hizi Kwa Mara Ya Kwanza

Kampuni ya simu janja ya Infinix ina matoleo mbalimbali yenye kufahamika kama Smart series, HOT series, NOTE series na Zero series, kila series ikipewa nguvu Zaidi katika kategori/feature fulani lakini sasa huenda ikawa ni tofauti kwa simu hii ya Infinix HOT 12.

Kwa taarifa za ndani kabisa ni kuwa simu hii inayotarajiwa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa tano kuja la ladha mpya kabisa kuanzia umahiri wa processor, Ram na Wat ya Chaji.

Simu hii inatarajiwa kuwa na teknolojia ya kuongeza RAM, inasemekana itaweza kuongeza Hadi 7GB RAM kitu kitakachoifanya kuwa toleo la HOT la kwanza kuwa na RAM kubwa zaidi hivyo kuifanya iwe na Kasi kiutendaji Kuliko matoleo yote ya HOT.

Simu hii inatarajiwa kuja na sifa kubwa kwa upande wa speed ya processor aina ya MediaTek na kasi yake ya gaming ni 85 na hii kuifanya kuwa simu ya kwanza ya toleo la HOT kuwa na processor yenye kuchakata kazi kwa haraka zaidi.

Simu za Infinix Zilizofanya Vizuri Sokoni Mwaka 2022

Tembelea @infinixmobiletz au piga namba 0743558994 kufahamu Zaidi kuhusu simu za Infinix.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.