Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Hatua za kufuata ili kuepusha kuuziwa simu used ambayo ni mbovu
Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu) Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Ni wazi kuwa kuna wakati mtu huwezi kununua simu mpya kutokana na sababu mbalimbali na hii hufanya chaguo lako kubakia kununua simu used au simu iliyotumika.

Lakini ni wazi kuwa kutokana na wimbi la udanganyifu ambalo limezidi sana siku hizi ni ngumu sana kuweza kupata simu nzuri used ambayo haina tatizo lolote, kuliona hili leo kupitia makala hii nimekuletea njia bora ambayo unaweza kutumia kununua simu used ambayo ni bora na ambayo haina tatizo lolote.

Siku za karibuni nimetumia njia hii kuweza kusaidia mtu kuweza kugundua kuwa simu nyingi za Galaxy Note 8 ambazo unaziona zimetapakaa sana kwa sasa, sio simu mpya bali ni simu used na wakati mwingine huwa na matatizo mbalimbali. Basi baada ya kusema haya moja kwa moja twende kwenye njia hizi.

Advertisement

Kwa kuanza labda ningependa kukupata tahadhari kuwa ni muhimu kununua simu kwenye maduka mbalimbali yanayo uza simu na sio kwenye mitandao ya kuuza na kununua. Hii itakusaidia sana kuweza kurudisha bidhaa pale itakapo kuwa na tatizo tofauti na unapo nunua kwa mtu binafsi kupitia mitandao hii.

Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Lakini kama umejikuta ni lazima kununua simu kwenye mitandao hii ya kuuza na kununua basi hakikisha unatumia njia hizi ili kuweza kujua kama simu unayo nunua inao ubora unao takiwa.

Njia ya Kwanza

Kwa kuanza njia hii ya kwanza inahitaji muda kidogo na hakikisha muuzaji anakupa muda wa kutosha kuweza kuangalia simu hii kwa undani. Mara nyingi matatizo ya nje ya simu huwa ni machache ukilinganisha na matatizo ya ndani.

Sasa baada ya kuangalia simu kwa nje na kujirithisha kuwa simu hiyo ipo kwenye muonekano mzuri basi moja kwa moja unachatakiwa kufanya ni kuunganisha simu hiyo na Internet kisha download app hapo chini kwenye simu hiyo unayotaka kununua.

Download App Hapa

Baada ya kudownload na ku-install vizuri app hiyo kwenye simu hiyo moja kwa moja fuata maelekezo hapo chini.

Kwa kuanza fungua app hiyo kisha bofya Menu iliyopo upande wa kushoto juu, kisha baada ya hapo chagua sehemu ya Start guided test.

Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa mwingine ambapo sasa unatakiwa kuchagua vitu unavyotaka kutest, unaweza kuchagua vitu vyote kwa kubofya na kuweka kiti kwenye chumba cha kila kitu unachataka kujaribu kwenye simu yako.

Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Baada ya hapo moja kwa moja bofya Test Phone, iliyopo mwisho kabisa wa ukurasa huo, kisha malizia kwa kukubali vigezo na mashart kwa kubofya OK na moja kwa moja utaweza kuanza kuona majaribio ya simu yako yakianza.

Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Hakikisha unafuata maelekezo yote kwenye kila ukurasa na mara baada ya kumaliza jaribio husika kama kila kitu kipo sawa bofya OK kuendelea kwenye jaribio linalifuata. Kama kitu hakipo sawa basi bofya Nok.

Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Kwa kufuata hatua zote hadi mwisho utaweza kupata ripoti ambayo itakuonyesha kama simu hiyo unayotaka kununua ni nzima au sio nzima. Kumbuka app hii haitaji Internet hivyo unaweza kutumia bure kabisa bila kuwa na bando mara baada ya kuinstall.

Njia ya Pili (Samsung)

Kwa kutumia njia hapo juu utaweza kujaribu simu hata kama ni Samsung au simu yoyote lakini njia hii ya pili ni bora sana kwa watumiaji wa simu za Samsung au kama unataka kununua simu ya Samsung.

Unachotakiwa kufanya ni kudownload app hapo chini kisha install kwenye simu yako vizuri alafu fungua na fuata maelezo hapo chini.

Download App Hapa

Kwa kuanza fungua app hiyo kisha bofya sehemu ya menu iliyopo juu upande wa kulia, kisha bofya sehemu ya Refurbishment Check. Sehemu hii itakusaidia kujua kama simu yako imebadilisha sakiti au firmware yake na kuwekewa firmware tofauti. Hii itakusaidia sana kwani simu zilizobadilisha hivyo mara nyingi zinakuwa na matatizo mengi ya software.

Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Baada ya hapo utaweza kuletewa ajibu kama simu yako imechezewa kwenye maswala ya software utaweza kuletewa ujumbe unao kwambia simu yako ni Refurbishmed, Kama simu yako haina tatizo upande huo utaweza kuetewa ujumbe kama huo hapo chini.

Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Kujua Kama simu Imebadilishwa Kava

Kutumia simu ambayo imefunguliwa kunakuweka kwenye hatari kwani hujui kama simu hiyo imebadilishwa nini na hujui kama hicho kitu kitadumu kwa muda gani. Kuepusha matatizo ya mara kwa mara jaribu kutumia njia hii ili kujua kama simu yako imefunguliwa.

Fungua app uliyopakua hapo juu, hakikisha unaweka Seriel number kama unatumia simu yenye mfumo wa Android 10 na kuendelea, unaweza kubofya sehemu ya Statu na kisha copy serial number ya simu yako na weka kwenye app.

Baada ya hapo utaweza kupata ripoti na ripoti ya kwanza ambayo ipo kwenye tab ya General itakuwa na maelezo ya Brand ya simu yako ikiwa pamoja na maelezo mengine. Kwenye ukurasa huo huo mwisho kabisa utaweza kuona sehemu ya Color / Internal.

Njia Bora ya Kununua Simu Used (Bila Kuuziwa Simu Mbovu)

Hakikisha sehemu hii inayonyesha rangi ya simu inayo fanana na simu yako kwani sehemu hii ikisema black alafu simu yako ni white basi jua kuwa simu yako imebadilishwa kava. Sehemu hii uweza kusoma data za ndani ya simu ambazo zimewekwa na Samsung.

Kwa kufuata hatua hizi moja kwa moja utaweza kununua simu ambayo ni simu bora ambayo haina matatizo yoyote. Kumbuka chukua muda wako kukagua simu kwa makini kwani mtu yoyote anae kuuzia simu kwa haraka basi lazima simu hiyo itakuwa na tatizo au sio halali. Kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua hatua za kufuata kama unataka kununua simu nzuri ya Android.

Natumaini makala hii inaweza kusaidia kununua simu used ambayo sio mbovu. Kama kuna mahali umekwama au unataka maelezo zaidi unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

3 comments
    1. wana boa sana nibora wangekua wanatuambia majina ya hizo app kuliko kusema download hapa ????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use