in

Hatua za Kufuata Kabla ya Kununua Simu ya Android (2021)

Ukizingati mambo haya na kuhakikishia utapata simu bora ya Android

Kununua simu ya Android
Photo by The Habari

Mwaka 2021 ni mwaka wa Smartphone, mpaka sasa tumesha ona kampuni mbalimbali zikijipanga kuleta mapinduzi ya teknolojia kwa upande wa simu za mkononi. Kutokana na kampuni nyingi kuingiza simu mbalimbali sokoni je unajuaje simu nzuri ya kununua, ni hatua gani ufutate kabla ya kununua simu..? tena kwenye mwaka huu wa simu janja.

Kama umekua ukijiuliza maswali hayo kwa muda mrefu, Tanzania Tech tunayo majibu. Hapa utaenda kujifunza ni mambo gani ya muhimu ya kuangalia wakati unanunua simu ya Android mwaka huu 2021. Tunajua simu za android ni nyingi sana sokoni pengine kuliko simu zingine zozote sasa kupitia hapa utaweza kujua ni simu gani itakayo kufaa kwa mwaka huu 2021, bila kupoteza muda twende tukajifunze hili.

1. Teknolojia Mpya

Kwanza ni anze na pointi hiyo ambayo ni ya msingi sana, kadri miaka inavyo zidi kwende teknolojia ya simu janja inazidi kubadilika. Hii ikiwa pamoja na muonekano wa simu mpaka ndani ya simu yani sifa za simu. Sasa ili uweze kununua simu yenye uwezo mzuri na simu itakayo dumu ni lazima kuhakikishe una nunua simu yenye teknolojia ya kisasa. Hapa na maanisha kuanzia kimfumo mpaka kisifa.

Kufafanua zaidi labda ni kwambie ni vitu gani usifanye, usinunue kamwe simu ambayo inatoleo la Android kuanzia Android 5.0 kushuka chini, Tafuta simu ambayo inatoleo kuanzia Android 6.0 na hii ni kwa sababu matoleo ya Android yanabadilika kila mwaka na matoleo ya zamani yanazidi kuondolewa na watengenezaji wa programu nyingi, hapa nikiwa na maanisha programu nyingi zitakuwa hazifanyi kazi kwenye matoleo hayo ya zamani hivyo ni muhimu kuhakikisha unatumia simu inayo endana na wakati.

Kwa namna nyingine kama unao uwezo ninge pendekeza ununue simu yenye mfumo wa Android kuanzia Android 7.0 na hii ni kwa sababu mfumo huu ndio unao shika chati kwenye simu nyingi za sasa na ndio mfumo unao semekana unatumika sana kwa sasa hivyo watengenezaji wa programu za Android mara nyingi wana hakikisha mfumo huu unafanya kazi vizuri kwenye programu zao.

2. Uwezo wa RAM

Hili nalo lipo kwenye teknolojia, lakini nimeona niliweke peke yake sababu unatakiwa kuelewa zaidi kuhusu RAM. Ukweli ni kuwa watu wengi hawazingati RAM pale wanapo taka kununua simu hasa simu za Android, lakini ningependa nikujuze RAM ni sehemu muhimu sana kwenye simu yako. Kama umekua ukipata matatizo ya simu yako kukwama-kwama (kustack) mara kwa mara au programu kufunga bila wewe kufunga mara nyingi hili husababishwa na RAM ya simu yako kuwa na uwezo mdogo.

Jinsi ya Kupakua Nyimbo Mpya za Bongo Flava za Hivi Sasa

Hapa tunarudi tena kwenye point ya juu ambayo ni kuhakikisha unanunua simu yenye toleo jipya la Android. Na hii ni sababu mara nyingi simu zenye toleo jipya la Android zinakuja na RAM ambayo ni kubwa kidogo ukilinganisha na simu zenye matoleo ya zamani.

Na hii huchangia kwenye simu yako kufanya kazi vizuri na kwa haraka sababu mara nyingi watengenezaji wa programu za Android huangalia mifumo mpya, hivyo kama utaona programu flani haifanyi kazi vizuri kwenye simu yako hii ni kutokana na watengenezaji wa programu hawakuzingatia simu zenye mifumo ya zamani hivyo programu hiyo inakuwa haiwezi kufanya kazi vizuri kwenye simu yako.

Na kumbuka ukubwa wa RAM mara nyingi hulandana na uwezo wa Processor kwa sababu Uwezo wa processor unategemeana sana na uwezo wa RAM, hivyo RAM Ikiwa na uwezo mkubwa basi lazima na processor nayo itakuwa na uwezo mkubwa.

3. Ukubwa na Uwezo wa Kioo

Ukubwa wa kioo pengine ni kitu ambacho unaweza ukasema sio sehemu ya muhimu, lakini mimi nitakwambia kwa sababu gani ni muhimu. Kwa upande wa uwezo wa kioo, ningependa nikwambie kuwa mara nyingi uwezo wa kioo chako unategemeana sana na kudumu kwa simu yako. Mara nyingi unakuta unanunua simu ndani ya mwezi umeangusha kidogo tu basi kioo kimesha pasuka na hii ni kutokana na uwezo wa kioo cha simu yako.

Mara nyingi vioo vyenye teknolojia ya zamani huwa ni vyepesi sana kupasuka na hii ni kutokana na kuwa mwanzoni kampuni wakati zinatoa simu hizo zilikuwa hazija gundua teknolojia hizo mpya au hazikuwa na uwezo wa kuweka teknolojia hizo mpya kwenye simu.

Sasa pale siku zinapo zidi kwenda ndipo kampuni mbalimbali zinagundua teknolojia mpya za vioo pamoja na kuwa na uwezo zaidi wa kuziboresha baada ya kupata fedha kutokana na mauzo. Pia vilevile mara nyingi kampuni hizi za simu husikiliza maoni ya watumiaji hivyo kuboresha vioo hivyo kadri siku zinavyo kwenda.

Sasa kwa upande wa ukubwa wa kioo ni kuwa, mara nyingi watengenezaji wa programu mbalimbali za android hufikiria kuunda programu zao kwenye simu zenye kioo kikubwa, na hii ni kwa sababu kwa sasa hakuna simu yoyote yenye uwezo mkubwa inayoingia sokoni ikiwa na kioo kidogo, hivyo ni muhimu sana kuchagua kioo kikubwa cha wastani na hiyo itakuwezesha kufurahia zaidi simu yako ya Android.

4. Uwezo wa Battery

Battery ni kitu ambacho watu wengi sana wamekua wakizingatia wakati wa kununua simu janja, lakini ningependa nikwambie watu wengi sana huangalia hili kwa utofauti. Hii ni kwa sababu watu wengi huangalia ni muda gani simu inaweza kudumu na chaji na kusahau kuangali uwezo halisi wa battery ya simu. Kudumu kwa chaji ya simu na uwezo wa battery ya simu ni vitu viwili tofauti na hii inatokana na kuwa kudumu kwa chaji kuna sababishwa na mambo mengi sana ikiwa pamoja na utumiaji wa simu, mara ngapi umechaji battery yako pamoja na mambo mengine kama hayo.

Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia

Lakini sasa kujua uwezo halisi wa battery yako ni lazima ungalie kipimo cha battery yako yani hapa na zungumzia zile (mAh) au kwa kitaalamu hizi huitwa “milliampere hour.” hii maana yake ni kipimo ambacho hutumiwa kupima uwezo wa battery. Mara nyingi kipimo hichi ndio kinaweza kutambua kuwa battery yako inauwezo gani, na hii ikiwa haijalishi ni mambo gani unafanya kwenye simu yako.

Sasa unaweza kujiuliza utajuaje hichi kipimo..? Mara nyingi watu wanapo enda kununua simu hasa za android utasikia wakiuliza “inakaa na chaji kwa mda gani..?” na kusikiliza muuzaji anachosema.. Guys!.. Please. muuzaji anachotafuta ni kufanya biashara hivyo atakwambia chochote kile unachotaka kusikia ili mradi ununue simu hiyo.

Sasa badala ya kumuuliza muuzaji chukua boksi la simu hiyo unayotaka kununua kisha geuza nyuma ya boksi hilo kisha soma kwenye maelezo, utakuta mahali pameandikwa namba ikifuatiwa na alama za mAh. (mfano Battery 3200mAh ), hiyo ndio njia pekee unayoweza kujua uwezo wa battery ya simu ya Android unayo taka kununua. Kumbuka namba hizo zikiwa kubwa zaidi ya 2500 ndio uwezo zaidi wa battery ya simu yako.

5. Mengine

Mambo mengine yaliyo baki sio ya msingi sana sababu haya hubebwa na jinsi mtu unavyotaka mwenyewe, kwa mfano Kuhusu ulinzi sio pointi ya msingi sababu kujilinda hii utegemeana na wewe mwenyewe pamoja na ulinzi utakao kwenye simu yako, simu inaweza ikawa na fingerprint lakini mtu akaweza ku-format fingerprint yako na kuingia ndani ya simu hiyo.

Ziko programu nyingi zenye uwezo wa kufanya hivyo. Kuhusu kamera sio jambo la msingi sana maana kamera haiwezi kufanya simu yako kushindwa kufanya kazi kwenye programu mbalimbali, unless wewe ni mpenzi wa picha au mpiga picha.

You see!.. ukweli ni kwamba hayo hapo juu ndio mambo ya msingi ya kuangali wakati unataka kununua simu yako ya Android kwa mwaka huu 2021. Sasa kama utakuwa umefanikiwa kusoma makala hii nzima, kwanza nikupongeza na nahakika utakuwa umejua ni nini cha kufanya kabla ya kununua simu yako mpya ya Android. Kwa makala zaidi hakikisha unaendelea kutembele Tanzania Tech kila siku, na kama una maoni maswali au ushauri usiite kutandikia kwenye maoni hapo chini.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

10 Comments

  1. Ok.asant.but simu yangu ni lg g3.inanisumbua sana siku iz inatabia nikiwa nimeishika mkononi kwa mda fulan au nikiweka mfukon kwa mda nakuta imejiwasha ikiwa imetoa mwanga wa kijan na tumaandish tudogo some time lang nyeus.blue ..tumaandish tupo kwa kingereza but inakera sana naaomba msaada