Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Makosa 5 Yanayofanya Battery ya Simu Yako Kuharibika

Rekebishe makosa haya kuweza kufanya Simu yako kudumu na chaji
smartphone-battery smartphone-battery

Linapokuja swala la battery ya simu yako kudumu na chaji hapa kuna mambo mengi sana yanayochangia, lakini pia kuna baadhi ya makosa ambayo tumekua tukiyafanya ambayo yanachangia sana kwa battery ya simu yako kutuwa na uwezo wa kudumu na chaji.

Kupitia Tanzania Tech leo tunakuleta makala hii ambayo utaweza kujifunza makosa 5 ambayo tunayafanya ambayo yanasababisha simu yako kutokudumu na chaji na kufanya battery ya simu yako kuharibika kabisa, bila kupoteza muda twende…

Advertisement

Kuchaji Simu Yako Kila Mara

Makosa 5 Yanayofanya Battery ya Simu Yako Kuharibika

Kuchaji simu yako kila mara ni moja kati ya kosa ambalo hufanywa na watu wengi sana, hapa  na maanisha unakuta mtu anachaji simu yake bila hata kujali simu imeisha chaji au lah!. Kwa mujibu wa utafiti battery za simu hupata maisha marefu na kudumu na chaji pale inapochajiwa ikiwa na asilimia 10 au asilimia 20. Hii hufanya battery yako kuongeza kiasi cha battery Charge circles ambacho ndio kufanya battery yako kudumu zaidi.

Kuchaji Simu Yako kwa Chaji Isiyo Sahihi

Makosa 5 Yanayofanya Battery ya Simu Yako Kuharibika

Chaji za siku hizi zimekua zikifanana, lakini pia hii haimanishi unaweza kutumia chaji yoyote kuchaji simu yako kwani kwa kufanya hivyo kuna hatari kubwa ya kuweza kuharibu battery yako. Mara nyingi pendelea kuchaji simu yako kwa kutumia chaji ya simu uliyonunulia kwani chaji hizi huwa zimepimwa na kudhibitishwa kuwa maalum kwa simu yako.

Kutumia Chaji Zinazodai Kuchaji Simu Yako Haraka

Makosa 5 Yanayofanya Battery ya Simu Yako Kuharibika

Mara nyingi watu wengi wamekua wakidai kuwa wanapenda aina flani ya chaja kwa sababu inachaji battery ya simu haraka. Hili sio sawa na inaweza kuharibu simu yako sababu mara nyingi chaji hizi hutoa umeme mkubwa kuliko inavyo staili. Badala yake hakikisha una angalia simu yako kama inayo teknolojia ya Fast Charging na hakikisha unanunua chaja yenye teknolojia hiyo pia.

Kuchaji Simu Huku Umeweka Kava kwenye Simu

Makosa 5 Yanayofanya Battery ya Simu Yako Kuharibika

Kutokana na simu zetu kuwa za bei ghali wengi wetu tumeweka cover protector kwenye simu zetu, lakini baadhi ya makava haya pia huchagia kwenye uharibifu wa batter zetu bila wenyewe kujua. Mara nyingi unapochaji simu yako unakuta umechaji huku kava liko kwenye simu yako, hii ni makosa makubwa sana na Uchangia kuharibu battery ya simu yako.

Battery inapochaji huwa inapata joto na simu nyingi zimetengenezwa maalum kuhimili joto hilo kutokana na uwekwaji wa sehemu za kupunguza joto hilo. Lakini mara nyingi kama unachaji simu yako huku umeweka kava linalo ziba kabisa simu yako unafanya sehemu hizo kushindwa kupunguza joto linalotokana na kuchaji simu yako na kusababisha battery yako kuharibika au kuvimba kwa joto kali.

Kuweka Wallpaper zenye Rangi Nyingi Angavu Sana

Makosa 5 Yanayofanya Battery ya Simu Yako Kuharibika

Hii najua itakuwa ni kitu cha kushangaza kwako lakini hichi ni chanzo kikubwa cha battery yako kuisha chaji kwa haraka. Mara nyingi unapokuwa umeweka picha yenye rangi nyingi angavu, simu yako kutumia chaji ya zaidi kuweza kukuonyesha rangi zote hizo kwenye kioo chako.

Hivyo basi mara nyingi kama unataka simu yako idumu na chaji pendelea kutumia Wallpaper zenye rangi moja au kama simu yako imeisha chaji na unataka idumu zaidi basi badilisha wallpaper yako na weka wallpaper yenye rangi nyeusi na utaona mabadiliko makubwa.

Kufanya simu yako idumu na chaji zaidi unaweza kusoma hapa, njia nyingine za kuweza kufanya simu yako kudumu na chaji kwa muda mrefu. Na hayo ndio baadhi tu ya mambo ambayo tumekuleta leo, je wewe unaonaje ni jambo gani lingine ambalo watu hufanya ambalo linaharibu battery za simu zetu..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

2 comments
  1. Ni kweli kabisa hususan iyo nanba 5 nimeikubali kwa 100% vipi nitaweza kufanya nn ili cmu yangu iweze tunza chaji Kama awali????

    1. Unaweza kutafuta kupitia Tanzania Tech, utaona makala inayohusu jinsi ya kufanya simu idumu na chaji zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use