Tengeneza Muziki kwa Kutumia (AI) Artificial Intelligence

Utaweza kutengeneza nyimbo mpya kwa kuchanya nyimbo zaidi ya moja
Tengeneza Muziki kwa Kutumia (AI) Artificial Intelligence Tengeneza Muziki kwa Kutumia (AI) Artificial Intelligence

Ni wazi kuwa teknolojia ya (AI) au Artificial Intelligence ndio teknolojia ambayo inatarajiwa kuendelea kutumika kwa kiwango kikubwa sana kwa miaka ya karibuni.

Hii ni kutokana na kuwa vitu vingi unavyovitumia sasa vinatengenezwa au vinatumia mfumo wa (AI) au Artificial Intelligence ili kufanya kazi kwa usahihi. Kuliona hili kupitia hapa Tanzania tech tutaendelea kukuletea njia mbalimbali za kutumia (AI) au Artificial Intelligence.

Mara baada ya kuonyesha njia ya kuandika kwa haraka kwa kutumia mfumo wa (AI) au Artificial Intelligence, siku ya leo tumekuletea njia mpya ya kutengeneza muziki kwa kutumia teknolojia hiyo.

Advertisement

Basi bila kupoteza muda twende kwanza niku onyeshe jinsi ambayo mimi nimefanikiwa kutengeneza (mashup) au muungano wa nyimbo mbili kati ya nyimbo mpya ya “kufuli ya Nandy” na nyimbo mpya ya “Bia Tamu ya Marioo” na kutengeneza muziki wa Kufuli Tamu ???? yote kwa kutumia AI.

Basi kama wewe unataka kutengeneza nyimbo kama hiyo au muziki kwa ujumla basi moja kwa moja endelea kwa kusoma hapo chini.

Kwa kuanza moja kwa moja tembelea tovuti hapo chini, unaweza kutumia smartphone au unaweza kutumia kompyuta.

Tembelea Tovuti Hapa

Baada ya kutembelea tovuti hii, moja kwa moja bofya kitufe cha create kilichopo kati kati ya tovuti hii.

Tengeneza Muziki kwa Kutumia (AI) Artificial Intelligence

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa kuchagua ni kitu gani ambacho unataka kufanya, kwa sasa unaweza kutengeneza Mashup ambayo unaweza kuchanganya nyimbo mbili tofauti, au pia unaweza kutengeneza Mixtape ambayo unaweza kuchanganya nyimbo nyingi tofauti.

Tengeneza Muziki kwa Kutumia (AI) Artificial Intelligence

Kama unataka kutengeneza video kama ambayo nimetengeneza mimi hapo juu, unaweza kuchagua sehemu ya Mashup.

Kisha baada ya hapo moja kwa moja ingia kwenye mtandao wa YouTube na tafuta video unazotaka kuchanganya copy link ya kwanza kisha paste sehemu ya Add YouTube songs or paste a link.

Tengeneza Muziki kwa Kutumia (AI) Artificial Intelligence

Baada ya hapo bofya sehemu ya Create Mashup kisha subiri baada ya muda mfupi utaweza kuona video yako ambayo itakuwa imesha changanywa moja kwa moja na itakuwa kama nyimbo moja. Pia unaweza kutengeneza audio pekee kwa kuchanganya audio mbili kutoka mtandao wa Spotify.

Sasa unaweza kujiuliza vip unaweza kuweka nyimbo hizi kwenye YouTube..? Kwa sasa bado haikubaliki kuweka nyimbo hizi kwenye mtandao wa YouTube kutokana na Copyright.

Lakini kuna wakati mwingine unaweza kuruhusiwa kuweka nyimbo hizi kwenye mtandao wa YouTube bila kuwasha Monetization kwenye video husika.

Bila shaka nitakuwa nimejibu maswali yako ya muhimu, kama unataka kujifunza zaidi kuhusu (AI) au Artificial Intelligence kwa ujumla basi endelea kutembelea Tanzania Tech.

Pia kupitia channel yetu hakikisha una subscribe kwani tunamalizia Studio zetu tayar kuanza kukuletea video zenye ubora kuhusu teknojoia na mambo mengine mbalimmbali.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use