in

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Zero X Pro

Zifahamu hapa sifa za simu mpya ya Infinix Zero X Pro

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Zero X Pro

Kampuni ya Infinix hivi leo imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Infinix Zero X Pro, simu hii ni moja kati ya simu iliyo zungumziwa sana kipindi cha karibuni na pia ni moja ya simu bora ya Infinix kuzinduliwa hadi sasa.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia baadhi ya sifa za simu hii mpya ya Infinix Zero X Pro, ikiwa pamoja na upatikanaji wa simu hii, bila kusahau kwanini nimekwambia simu hii ni bora kutoka Infinix hadi sasa. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Sifa za Infinix Zero X Pro

Zifuatazo ni baadhi ya sifa za simu mpya ya Infinix Zero X Pro, kumbuka sifa hizi zinaweza kuongezeka zaidi pale simu hii itakapo toka rasmi hapa Tanzania.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Zero X Pro

Muundo

Kwa kuanza na muundo, simu hii imetengenezwa kwa Glass mbele na nyuma, kwa pembeni simu hii inakuja na frame ya plastic. Hii inafanya simu nzima ya Infinix Zero X pro kuwa na uzito wa hadi gram 193 g ambayo ni sawa na kilogram 0.193 kg.

Simu hii inakuja na mumbo la box, ikiwa ni na mikunjo au mikato kwenye kona kwa juu na chini.

Kioo

Tukiangalia kioo simu hii kinakuja kimetengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED huku kikiwa na ukubwa wa inch 6.67, kioo hichi kina uwezo wa resolution ya hadi pixel 1080 x 2400. Kioo hichi pia kinakuja na uwezo wa refresh rate ya hadi 120Hz, pamoja na uwezo wa mwanga au nits 700 (peak).

Mbali na hayo, kioo cha Infinix Zero X Pro pia kimeficha sehemu ya Fingerprint ambayo inapatikana chini ya kioo.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Sifa za Ndani

Kwa upande wa sifa za ndani, Infinix Zero X Pro inakuja na Processor inayo endeshwa na chipset ya Mediatek Helio G95 yenye CPU ya hadi 2×2.05 GHz Cortex-A76 & 6×2.0 GHz Cortex-A55 Octa Core. Kafanya ufungue Apps na Games bila wasiwasi, Zero X Pro inasaidiwa na RAM ya hadi GB 8.

Mbali ya hayo simu hii inakuja na aina mbili za ROM au uhifadhi wa ndani, huku uhifadhi mkubwa ukiwa ni GB 256 na chaguo lingine ikiwa ni GB 128. Kama uhifadhi huu hautoshi kwa matumizi yako unaweza kuongeza uhifadhi kupitia sehemu ya Micro SD Card ambayo inajitegemea.

Kamera

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Zero X Pro

Kwa upande wa kamera Infinix Zero X Pro inakuja na kamera tatu kwa nyuma, kamera kuu ikiwa na Megapixel 108 na nyingine mbili zinakuja na Megapixel 8 kila moja. Kamera hizi kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video za hadi 4K, huku ukiwa na uwezo wa kuzoom hadi X60.

Kusaidia kamera hii hasa wakati wa usiku, Zero X Pro inakuja na flash za Quad-LED flash, pamoja na teknolojia nyingine kama HDR, pamoja na panorama.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Zero X Pro

Kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja yenye Megapixel 16, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080 kwa frame 30 kwa sekunde. Kamera hii pia inasaidiwa na flash za Dual-LED flash

Viunganishi

Kwa upande wa viunganishi Zero X Pro inakuja na sehemu ya USB Type C toleo la 2, tundu la kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, pamoja na sehemu ya kuweka line mbili za Nano SIM, bila kusahau sehemu ya kuweka memory card ya Micro SD Card ambayo inajitegemea.

Pia kwa kuongeza simu hii mpya ya Infinix Zero X Pro inakuja na Radio FM, GPS, Bluetooth toleo la 4.2 au toleo la 5.0, WiFi pamoja na Hotspot.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Battery

Kwa upande wa battery simu hii inakuja na battery ya mAh 4500, huku ikiwa na uwezo wa kuchajiwa na chaja yake yenye teknolojia ya Fast charging yenye 45W. Kwa mujibu wa Infinix, chaja hii ina uwezo wa kujaza simu hii hadi asilimia 40% kwa dakika 15.

@tanzaniatech

Infinix Zero X Pro Unboxing.. link kwenye.bio to learn more#tanzaniatech #maujanja #infinix #zeroxpro #zerox #smartphone #tanzania #tech

♬ Swear By It – Clutch

Upatikanaji

Kwa upatikanaji, Simu hii inatarajiwa kuanza kupatikana hapa Afrika kwa nchi ya Nigeria kwanza, na baadae kupatikana kwa nchi nyingine. Utaweza kupata simu hii kwa rangi tatu tofauti yaani Nebula Black, Starry Silver, na Tuscany Brown. Kama unataka kujua zaidi kuhusu bei unaweza kusoma hapa.

Simu Bora kutoka Infinix

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Zero X Pro

Sasa kwa maoni yangu ambayo yana angalia zaidi sifa za simu hii, Infinix Zero X Pro ni toleo bora la Infinix kutokana na teknolojia iliyo tumiwa kwenye kamera kwa kuweka 60X Pericope lensi, pia muonekano wa simu hizi ni tofauti kabisa na simu zote za Infinix ambazo zimezinduliwa hadi sasa.

Bila kusahau aina ya kioo ambacho kimetumika ambacho ni AMOLED, pia pamoja na teknolojia ya Fast charging ya hadi 45W. Japo kuwa awali ilitangazwa kuja na chaja ya 160W.

Kwangu mimi kwa sababu sijashika simu hii nadhani hayo ndio machache yanayofanya nione simu hii ni bora pengine kuliko matoleo mengine ya simu za Infinix ambayo yamepita. Vipi wewe kwa maoni yako unasemaje kuhusu simu hii kwa kuona sifa zake.? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.