in

Pima Mapigo ya Moyo kwa Kutumia Smartphone Yoyote

Utaweza kujua mapigo yako ya moyo kwa kutumia simu yako

Pima Mapigo ya Moyo kwa Kutumia Smartphone Yoyote

Afya ni kitu cha msingi sana kwani kuwa na afya njema ndipo kunatupa nafasi ya kuendelea kuishi na kuendelea kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia. Kuliona hili leo nimeona nikuletee makala fupi yenye kuonyesha njia rahisi ya kufanya huduma ya kwanza ya kupima mapigo ya moyo kwa kutumia Smartphone yoyote.

Kumbuka njia hii haibadilishi umuhimu wa kwenda hospitali kama unajisikia utofauti kwenye mwili wako kwa namna yoyote. Njia hizi ni kwa ajili ya kujifunza hivyo ni muhimu kumuona daktari pale unapohisi dalili yoyote ya ugonjwa kwenye mwili wako.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Basi baada ya kusema hayo twende moja kwa moja kwenye njia hii, Njia hii inahusika app ambayo binafsi nimeifanyia uchunguzi kwa muda mrefu na kila mara nimeona app hiyo inatoa vipimo ambayo ni sahahi au vinakaribiana na usahihi wa kipimo cha mapigo ya moyo kilichopo kwenye saa janja au smartwatch ya Apple (Apple Watch).

Jinsi App hii inavyofanya kazi inapima jinsi damu inavyopita kwenye mishipa ya damu ya kidole chako kwa kutumia kamera ya nyuma ya simu yako.

Kama uniamini unaweza kujaribu app hii kwa kudownload kupitia link hapo chini, App hii inapatikana kwenye mifumo yote ya Android pamoja na iOS.

Mfumo wa Android

Download App ya Kwanza Hapa

Download App ya Pili Hapa Android

Mfumo wa iOS

Download App Hapa iOS

Unatakiwa kudownload app hiyo kisha install vizuri kwenye simu yako alafu fuata maelekezo ya kwanza kisha weka kidole kwenye sehemu ya kamera ya nyuma ya simu yako kisha bofya kitufe cha BEGIN MEASUREMENT, baada ya hapo subiri mpaka uviringo maalum unaonekana kwenye kioo chako ujae kisha utaweza kuona kiwango cha mapigo ya moyo wako.

Na hiyo ndio njia rahisi ambayo unaweza kutumia kupima mapigo ya moyo kwa kutumia smartphone yoyote, Kumbuka kama unataka kujua apps nyingine za kukusaidia kiafya unaweza kusoma makala hii ya apps nzuri kwa ajil ya Afya yako.

Kwa maujanja zaidi pamoja na jinsi ya kujua apps nzuri za kutumia kwenye simu yako ya Android hakikisha una subscribe kwenye YouTube channel yetu ya Tanzania Tech hapa.

Pima Mapigo ya Moyo kwa Kutumia Smartphone Yoyote
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments