in

Infinix Yazindua Simu Mpya ya HOT 10T Yenye Ofa Mpya

HOT 10T inapatikana ikiwa na ofa ya kifurushi cha GB 78 kutoka Tigo

Infinix Yazindua Simu Mpya ya HOT 10T Yenye Ofa Mpya

Infinix HOT 10t ni simu mpya kutoka toleo la HOT. Infinix HOT 10t sifa kuu ni G70 processor na kamera tatu kamera kuu ni MP48 vile vike simu hii ina battery ya mAh 5000 na wigo mpana wa koo cha nchi 6.82 90hz. Simu ya Infinix HOT 10t kwa sasa inapatika katika maduka ya simu nchini kote ikiwa na ofa ya GB78 kutoka Tigo. Tudadavue kwa undani faida ya kila sifa ya Infinix HOT 10t.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kamera:

MP48+2+lens na MP8 ya camera ya mbele hufanya picha zilizochukuliwa na camera hizi kuwa ang’avu na zenye uhalisia kulingana na mazingira usika. flash ya Infinix HOT 10t husaidia katika nyakati za usiku kupata picha bora na za kuvutia.

Battery:

Infinix Hot 10t ina mAh 5000 za battery. Battery ya Infinix HOT 10t inakupa nafasi yakufanya vitu vingi kama vile kucheza games, kuangalia movie, kusikiliza music nakadhalika pasipo kukata chaji kwa zaidi ya masaa 24.

Memory:

GB4/64 ya HOT 10t inauwezo wa kuhifadhi vitu mbalimbali au naweza nikasema files nyingi kama files za picha, videos, vitabu vya kujisomea na hata application zenye uwezo wa kukaa kwenye memory card.

Infinix Yazindua Simu Mpya ya HOT 10T Yenye Ofa Mpya

Kioo:

kioo cha Hot 10t ni nchi 6.82 kimeambatana 90hz hii ni teknolojia yenye kukifanya kioo kiwe smooth pindi utaumiapo simu yako. Kioo hiki cha HOT 10t na 90hz huongeza ufanisi na wepesi wakati wa kuperuzi na kufungua application za simu.

Android:

Infinix HOT 10t inatumia Android 11. Android 11 ni nyepesi kutumia hata kwa yule aliyemgeni katika ulimwengu wa simu janja basi hawezi pata shida wakati wa kuitumia simu hii lakini pia Adroid 11 inaruhusu simu kupata update mpya za application.

Tigo ofa:

Infinix Yazindua Simu Mpya ya HOT 10T Yenye Ofa Mpya

HOT 10t inapatikana katika maduka ya simu ikiwa na ofa ya GB78 kwa mwaka, kupitia ofa hii utafurahia kasi ya internet ya 4G kutoka kwenye simu yako.

Infinix HOT 10 Play inapatikana katika maduka ya Tigo na Infinix nchini kote. Tembelea https://www.infinixmobility.com/tz/ au piga namba 0744606222.

Infinix Yazindua Simu Mpya ya HOT 10T Yenye Ofa Mpya
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix Kimataifa Yatwaa Tuzo 7 Katika Maonyesho Ya Ces 2024

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.