Je, Tunahitaji Uzoefu wa Kazi ili Kuweza Kuajiriwa.?

XTOK na mjadala wa Je, Tunahitaji Uzoefu wa Kazi ili Kuweza Kuajiriwa.?
Je, Tunahitaji Uzoefu wa Kazi ili Kuweza Kuajiriwa.? Je, Tunahitaji Uzoefu wa Kazi ili Kuweza Kuajiriwa.?

Imekuwa ikiwapa wakati mgumu sana hasa wale wanaokuwa wamemaliza masomo yao kwa muda mfupi na kuingia katika harakati za kutafuta ajira.

Ofisi nyingi sana hasa Mashirika Binafsi (yasiyo ya Kiserikali) na Makampuni binafsi yamekuwa yakiongeza suala la Uzoefu wa kazi kama kigezo cha kupata ajira.

Hivyo kampuni ya simu ya Infinix ikaona ni vyema kuwakutanisha vijana kutoka sehemu mbali mbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo kuweza kujadili suala hili kupitia mdahalo unaosema “Je, tunahitaji uzoefu wa kazi ili kuweza kuajiriwa.?” ambapo ilifanyika katika Ukumbi wa Sahara Ventures uliopo Morocco siku ya Jumamosi Tarehe 10/04/2021.

Advertisement

Je, Tunahitaji Uzoefu wa Kazi ili Kuweza Kuajiriwa.?

Mdahalo huu uliwataka vijana kujigawa katika vikundi viwili wenye kukubaliana na mada ambao walifahamika kama Kundi Black na kundi White wenye kupinga kwamba ili kuajiriwa uzoefu si kitu cha lazima. Mdahalo huu uliongozwa na watu Maarufu kama vile MC. Anthony Luvanda, Bi. Shamila Mshangama na Mr. Erick Benard (Mr. Ben)

Je, Tunahitaji Uzoefu wa Kazi ili Kuweza Kuajiriwa.?

Mchuano ulikuwa ni makali mno kuanzia kwenye vikundi hivyo viwili hadi kwa wageni waalikwa ambao ndio walikuwa kama majudge na waongozaji wa mdahalo mzima.

Bi. Shamila alianza kwa kuipinga mada “kupata kazi sio lazima uwe umeajiriwa maana unaweza kujiajiri kwa kuwa na taasisi ambapo unaweza kuonwa kutokana na juhudi ulizofanya, hivyo utakuwa umepata uzoefu kupitia hapo lakini hujaajiriwa”.

Lakini pia MC Luvanda aliikataa hoja kwa kusema “unaweza kuwa huna uzoefu wowote na bado ukafanya vizuri saana na mwenye uzoefu asifanye vizuri pia”.

Vijana wote katika makundi yao nao walionekana kuwa wamejiandaa vya kutosha kila upande ulkiwa na hoja zenye kujitosheleza iliyopelekea kutopata mshindi mmoja kwani kila mmoja aliibuka  kidedea na kuondoka na zawadi mbalimbali kama vile Simu, Tshirt, Wireless Keyboards za kompyuta pamoja na Note 8 package iliyokuwa na vitu mbali mbali kama (Mwamvuli, Notebook, Power bank, chupa ya chai/maji, zilizoandaliwa na Mdhamini Mkuu ambayo ni kampuni yenye kujihusisha na uzalishaji wa simu janja Infinix Mobile.

Infinix Pamoja ya kuwa ni kampuni iliyojikita kwenye soko la simu lakini pia ni kampuni yenye kumjali Zaidi mwanafunzi wa leo kwa kumuandaa kwajili ya kesho yake. Kupitia XTOK Infinix imeweza kuwafikia wanafunzi wengi sana kwa wakati mmoja ambapo kila mwanafunzi hujifunza kitu kipya katika Tafrija hii ya XTOK.

Je, Tunahitaji Uzoefu wa Kazi ili Kuweza Kuajiriwa.?

Infinix mobile Tz kuwaahidi vijana na wote walio hudhuria kwenye mdahalo huu kuwa watakuwa nao Pamoja kwenye shughuli zote za vijana na pia kuwasihi wasikose mdahalo ujao kwa kuwapa nafasi pia wao kuchagua mada ambayo itakuwa ya Xtok inayofata, mada inaendelea kwenye kurasa zao za kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter na pia kwenye kiunga chao cha Xclub.

Tembelea link hii kuona mdahalo huu ulivyoenda

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use