in

Kutengeneza Katuni Kutoka Kwenye Picha (2021)

Tengeneza katuni kutokana na picha zako kwa haraka bila kuwa na ujuzi wowote

Kutengeneza Katuni Kutoka Kwenye Picha (2021)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kubadilisha picha zako kutoka kwenye picha za kawaidia na kuzifanya kuwa kama katuni basi makala hii ni kwa ajili yako. Tofauti na njia nyingine ambazo zimezoeleka njia hii ni rahisi sana na unaweza kubadilisha karibia kila picha kwa urahisi.

Kama unavyoweza kuona, njia hii inafanya kazi kwa asilimia 100 na utaweza kuona picha hizo mbili ambazo nimezitoa mtandaoni tu na kuweza kujaribu njia hii rahisi. Kupitia njia hii huna haja ya kuwa na ujuzi wowote bali unahitaji kuwa na kompyuta tu na kama huna kompyuta basi unaweza kujaribu njia hii kupitia simu yako ya Android au hata iOS.

Bila kuendelea kupoteza muda zaidi basi moja kwa moja twende nikuonyesha hatua unazotakiwa kufuata. Kama unayo kompyuta basi fuata njia za kompyuta na kama huna kompyuta basi fuata njia za kutumia simu.

Tengeneza Katuni Kwa Kutumia Kompyuta

Kwa kuanza Bofya Hapo chini, kisha moja kwa moja pakua programu ya Prima Cartoonizer kwenye kompyuta yako. Kumbuka wakati unapakuwa programu hiyo chagua sehemu ya Download Prima Cartoonizer EXE file. Download programu hiyo kwenye kompyuta yako kisha install kwenye kompyuta yako na sasa washa programu hiyo.

Jinsi ya Kutumia Smartphone Yako Kama Microphone

Download Programu Hapa

Baada ya kuwasha bofya kitufe cha Add kilichopo upande wa kulia juu, chagua picha unayotaka kufanya iwe katuni. Baada ya kuweka picha hiyo angalia upande wa kushoto utaona Sample ya picha ambazo unaweza kufanya ziwe kama hivyo. Chagua aina ya katuni ambayo unapendelea zaidi na kisha subiri baada ya muda na utaona picha yako imekuwa katuni.

Kutengeneza Katuni Kutoka Kwenye Picha (2021)

Kama unavyoweza kuona hapo juu, hivyo ndivyo ambayo utaweza kubadilisha picha yoyote kuwa katunia kwa kutumia kompyuta yako. Baada ya kuridhika na aina ya katuni unaweza kuhifadhi picha yako moja kwa moja kwa kubofya kitufe cha Save juu katikati.

Tengeneza Katuni Kwa Kutumia Simu

Kama huna kompyuta usijali pia unaweza kutumia njia hii kwenye simu yako, iwe unatumia simu ya Android au iOS utaweza kufanya njia hizi kwa urahisi kabisa. Kwa kuanza unatakiwa kutembelea tovuti hapo chini, baada ya hapo bofya kitufe cha Choose File, kisha chagua picha unayotaka kubadilisha iwe katuni.

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

Tembela Tovuti Hapa

Baada ya hapo subiria kwa muda mfupi kidogo na utaweza kuona picha imebadilika kabisa na utaweza kuona picha yako imekuwa katuni kwa haraka na urahisi kabisa.

Kutengeneza Katuni Kutoka Kwenye Picha (2021)

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu huo ndio muonekano wa programu hiyo mtandaoni. Kwa sababu mimi nimetumia kompyuta unaweza kuona muonekano wa tofauti kwenye simu yako lakini na kuhakikishia utaweza kutengeneza katuni kwa haraka na urahisi bila kutumia muda mrefu. Natumaini umeweza kutengeneza katuni kwa kutumia simu au kompyuta yako.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuondoa background kwenye video yoyote kwa urahisi na haraka. Pia kama unataka unaweza kusoma hapa kuondoa background kwenye picha zako kwa haraka na bila kutumia programu yoyote.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment

  1. Habari
    Nina simu yangu Galaxy Note 4 ina tatizo la kuzima zima na kuwa ngumu kuwaka au mda mwingine ikiwaka inakaa downloading pia ikifika asilimia 50 inazima hivi lakin ikiwaka ukiwa unaitumia huwa haizimi hivi tatizo linaweza kuwa mashine inakaribia kufa, kuflash au battery