Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure)

Hatua kwa hatua jinsi ya Kumiliki tovuti yako kama ilivyo tovuti ya facebook
Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure) Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Tanzania Tech lazima unajua kuwa tumeshawahi kutengeneza tovuti kama ilivyo Twitter ndani ya muda mfupi sana, lakini siku ya leo nimekuletea makala nyingine ambayo tunaenda kuangalia jinsi ya kutengeneza tovuti kama ilivyo Facebook ndani ya muda mfupi sana.

Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure)

Unaweza kuangalia Mfano Hapa

Advertisement

Kwa kuwa baadhi ya hatua zinafanana na hatua zile za awali za kuinstall mfumo wa Twitter, basi moja kwa moja nitarudia baadhi ya maelezo ili kuokoa muda, pia kama unataka kuweza kuinstall website yoyote ni vyema kuendelea kufahamu hatua hizi muhimu sana.

Baada ya kuangalia mfano na kusema hayo, kitu ambacho unahitaji sasa ni kuchukua simu au kompyuta yako moja kwa moja, kisha twende kwenye hatu za jinsi ya kuinstall tovuti hii kwenye domain yako pamoja na hosting yako.

Kama kwa namna yoyote huna domain wala hosting basi unaweza kupata domain na hosting kwa urahisi kwa kufuta hatua hapa chini, hakikisha una anza kuangalia kuanzia dakika ya 7 na sekunde 34. Unaweza kubofya hapa na kuanza kuangalia video hiyo kwenye dakika hiyo.

https://youtu.be/C_G4WLBSCP0?t=447

Baada ya hapo unaweza kuendelea kwa kudownload file za tovuti hiyo ya Facebook hapo chini na kisha endelea kwa ku-upload file hizo kwenye domain yako kama ilivyo kwenye video hapo juu. Kumbuka unaweza kuanza kwa kuangalia kuanzia dakika ya 7 na sekunde 34.

Download Hapa

Baada ya kuweka file hizo sasa unaweza kuendelea kwenye hatua zifuatazo ambazo ni rahisi sana, hakikisha umetengeneza database na unazo password zake na username.

Kupitia browser yako andika jina la domain yako kisha andika /install mbele yake, mfano tanzaniatech.one/install hakikisha una andika kama ilivyo kwenye mfano huo. Baada ya kuandika hivyo utaweza kuona maelezo hayo hapo chini kwenye kioo cha simu au kompyuta yako.

Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure)

Fuata maelezo hayo kwenye kioo cha simu au kompyuta yako, maelezo hayo yapo kwa kiswahili hivyo natumaini kila mmoja ataweza kufuatilia maelezo hayo kwa makini na usahihi. Kitu cha muhimu ni kuhakikisha unakuwa na vitu hivi hapo chini.

  • Jina la Database Yako – Weka jina la database.
  • Username ya Database – Weka username ya database.
  • Password au Neno la Siri la database – Weka password ya database.
  • Jina la Host – Weka jina la host name hapa mara nyingi inakuwa ni localhost kama ni tofauti utapewa data hizi wakati wa kutengeneza database.
  • Namba ya Database Port – Namba ya Database Port mara nyingi namba hii huwa ni 3306 kama server yako inayo namba ya tofauti basi unaweza kuandika namba hiyo kwenye sehemu hiyo.
  • Barua Pepe yako (E-mail) – Andika email ya website yako (Hii ni barua pepe kuu ambayo ndio utatumia wewe kama admin.
  • Username ya Admin – Hii ni username ambayo ndio utakuwa unatumia wewe kama admin, hakikisha huandiki (Admin) kwani hii userame itakataa chagua userame nyingine sahihi.
  • Neno la siri (Password) – Andika password yako wewe kama admin na hii ndio itakayo tumika kwako wewe kama admin. Hakikisha password hii inakuwa herufi au namba zaidi ya sita, na sio pungufu ya hapo.

Baada ya kumaliza hatua zote hizo sasa utaweza kuona ukurasa wenye maelezo yote uliojaza kwenye vyuma vyote vilivyopita. Hakiki maelezo yako kama yako sahihi kisha malizia kwa kubofya Install ambayo ipo chini upande wa kulia.

Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure)

Baada ya hapo sasa unaweza kuingia kwenye tovuti yako kwa kutumia username na password yako uliyotengeneza hapo awali, unaweza kutumia email pia kama username yako.

Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure)

Baada ya hapo sasa ingia kwenye tovuti yako kisha bofya kwenye picha ya profile kisha chagua sehemu ya Admin Panel kwenye sehemu ya hii ndio sehemu ambayo hapo ndipo utaweza kuendesha kila kitu kwenye tovuti hii.

Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure)

Baada ya hapo unaweza kuendelea kwa kubadilisha baadhi ya vitu kupitia sehemu ya Admin Panel, kumbuka mfumo huu unao endeshwa na sehemu hiyo hivyo kila kitu kilichopo kwenye website hiyo kinaendeshwa kupitia sehemu hii ya Admin Panel.

Tengeneza Tovuti Kama Facebook Ndani ya DK 15 (Bure)

Sifa za Tovuti Hii

Kupitia tovuti hii unaweza kufanya mambo mengi sana ikiwa pamoja na mambo haya ambayo watumiaji wako wataweza kuyafanya

Watumiaji Wako Wataweza

  • Kuuza na Kununua Bidhaa
  • Kutengeneza Stories
  • Kuandika Blog
  • Kutengeneza Events
  • Kutengeneza Group
  • Kutengeneza Page
  • Kupost Kupitia Forum
  • Kupost Video
  • Kupost Picha
  • Kupost Link
  • Kupost Poll
  • Kuchat mtu mmoja na mwingine
  • Mtumiaji ataweza kupost matangazo kwa kulipia matangazo hayo kama ilivyo kwenye mfumo wa Facebook.
  • Na mambo mengine mengi..

Admin Utaweza Kufanya Haya

  • Utaweza kuweka tiki ya blue kwenye ukurasa unaotaka (ku-verifie profile)
  • Kuzima na kuwasha sehemu yoyote ya tovuti hiyo
  • Kufuta au kusitisha akaunti ya mtu yoyote au page, au group au even au picha au link au poll na vitu vingine vyote.
  • Ataweza kuseti kiasi cha pesa ambacho kila akaunti inakua nayo kwa ajili ya matangazo, hii ikiwa ni pamoja na kuchagua aina ya alama ya fedha unayotaka ionekane
  • Utaweza kuchagua lugha ya website
  • Utaweza kuzima website au kuiwasha kwa watu wote.
  • Na mambo mengine mengi…

Tovuti Hii Inawezaje Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Unaweza kutengeneza pesa mtandaoni kwa tovuti hii kwa kuwasha sehemu ya matangazo ambayo watu watakuwa wanalipia ili kuweza kuweka matangazo yako kwenye tovuti hii kama ilivvyo facebook. Pia unaweza kuweka matangazo ya Adsense kama utakuwa umechagua tovuti hii iweze kuwa na lugha ya kiiingereza.

Pia unaweza kufanya tovuti hii kuwa tovuti ya kulipia yaani mtu anatakiwa kulipia ndipo aweze kutumia tovuti hii kwa asilimia 100. Hii ni nzuri kwa mtu ambaye ametengeneza tovuti ambayo inafaida kwa watu kwa namna moja ama nyingine yaani kama vile website ya movie ambapo watu wata download au kuangalia movie, au mengine..

Hadi hapo natumani utakuwa umeweza kutengeneza tovuti yako kama ilivyo facebook,

Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani sasa tutakuwa tunaweka makala nyingi zaidi kila siku. Kama unataka kujifunza hatua hizi kwa video hakikisha unajiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech hapa.

Kwa muajanja zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza tovuti kama Twitter kwa haraka na urahisi ndani ya DK 15.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use