in

Picha Hii Inaweza Kuharibu Simu Yako (Usijaribu Tafadhali)

Tafadhali usijaribu hii kwenye simu yako hata kidogo

Picha Hii Inaweza Kuharibu Simu Yako (Usijaribu Tafadhali)

Katika ulimwengu huu wa teknolojia ni wazi kuwa hakuna hajuae kila kitu, hii inathirika kwenye picha moja ambayo imeanza kusambaa mtandaoni ambayo ina uwezo wa kuharibu simu yako na usiweze kutumia simu yako kabisa.

NOTE – Tafadhali usijaribu hii kwenye simu yako utaweza kuharibu simu yako kabisa, hatuta usika pale utakapo haribu simu yako.

Kwa mujibu wa tovuti ya 9to5google, picha hiyo ambayo ina muonekano wa anga wakati wa jioni, inauwezo wa kuharibu kabisa simu yako (Soft-bricked) pale utakapo weka picha hiyo kama wallpaper kwenye simu yako. Kwa mujibu wa tovuti hiyo simu nyingi ambazo zinaonekana kuharibika ni simu za Samsung, lakini hata simu nyingine za Android zinaweza kuaribiwa.

Kama unavyoweza kuna hapo juu kwenye video simu yako inaweza kuendelea kufanya hivyo hadi hapo utakapo fanikisha kuondoa wallpaper hiyo kwenye simu yako ya Android.

Hakikisha unakuwa makini na wallpaper hiyo hata pale mtu anapo kutumia kwenye simu yako kwani inaweza kuharibu simu yako. Kwa sasa bado sababu kamili za picha hiyo kuharibu simu za Android hazija julikana, ingawa kuna taarifa kuwa hii inatokana na baadhi ya mifumo ya Android kutokuwa na uwezo wa rangi zilizopo kwenye picha hiyo.

Kwa sasa hakikisha kuwa simu yako inakuwa salama na usiweke wallpaper hii kwenye simu yako hata kidogo. Kumbuka kuwa unaweza kuharibu simu yako moja kwa moja hivyo hakikisha kuwa HUJARIBU picha hii kwenye simu yako.

Njia Mpya ya Kutengeneza Pesa Kupitia YouTube Shorts Video

Kwa habari zaidi kuhusu ili hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech, tutakuleta taarifa zaidi pale tutakapo fahamu zaidi kwanini picha hii ina uwezo wa kuaribu simu nyingi za Android.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.