in

Jinsi ya Kutumia Hashtag Kupata Likes Nyingi Instagram

Hii hapa njia rahisi ya kupata likes kwa urahis kwa kutumia hashtag

Jinsi ya Kutumia Hashtag Kupata Likes Nyingi Instagram

Kama wewe ni mmoja kati ya watu ambao ni watumiaji wa mtandao wa Instagram, basi najua unajua sana kuhusu hashtag. Hashtag ni moja kati ya nyenzo muhimu sana kwenye mtandao wa instagram hasa kama unataka kufikia watu wengi zaidi.

Kupitia makala hii nitaenda kushare na wewe njia rahisi ambayo unaweza kutumia ili kufikia watu wengi na kupata likes nyingi kwenye picha na video zako kupitia mtandao wa Instagram kwa kutumia hashtag. Kumbuka njia hii inafanya kazi zaidi kama unataka likes na sio followers, kama unataka followers basi unaweza kusubiri makala yetu nyingine.

Kwa kuanza unachotakiwa kufanya ni kufuata njia hii hapa ili kujua muda ambao watu wengi zaidi wanatembelea akaunti yako au muda ambao watu wengi zaidi huwa mtandaoni kulingana na nchi uliyopo. Kama unataka kufikia watu kutoka nje ya nchi unaweza kuachana na hatua hiyo hapo juu na kwenda moja kwa moja kwenye hatua inayofuata.

Jinsi ya Kutumia Hashtag Kupata Likes Nyingi Instagram

Unacho takiwa kufanya ni kupakua app hapo chini inayoitwa Hashtag Generator, app hii ni tofauti kabisa na app nyingine ambazo umewahi kuzisikia. App hii inatumia mfumo maalum wa AI kuweza kujua ni aina gani ya hashtag ambazo unatakiwa kutumia kwenye picha au video ili kufikia watu wengi zaidi. Unaweza kupata app hiyo hapo chini.

Baada ya kupakua app hii sasa endelea kwa kufungua app hiyo kisha endelea kwa kuchagua maneno, au picha au link ya post ili kupata hashtag. Sehemu bora ni sehemu ya katika ambayo ni Photo, bofya hapa na kisha bofya “New Photo” alafu chagua picha ambayo unataka kupost kwenye akaunti yako ya Instagram alafu subiri baada ya muda app hiyo itakwambia ni hashtag gani ambazo ni bora kwako kutumia kwenye picha hiyo.

Jinsi ya Kutumia Hashtag Kupata Likes Nyingi Instagram

Baada ya hapo kupata matokeo mazuri, copy hashtag ambazo zinatokea kwenye sehemu ya medium na na sehemu ya Easy na kwenye sehemu ya hard copy hashtag moja tu. Hii ni kwa sababu hashtag za hard ni ngumu kufikia watu wengi kutokana na kutumiwa na watu wengi sana na hashtag nyingine ni rahisi kwani hazitumiwi na watumiaji wengi.

Kama unataka kucopy hashtag, bofya hashtag unazo zitaka kisha moja kwa moja bofya kutufe cha copy kinacho tokea upande wa kulia chini na moja kwa moja hashtag hizo zitacopiwa tayari kwa kuziweka kwenye post yako kwenye mtandao wa Instagram.

Jinsi ya Kutumia Hashtag Kupata Likes Nyingi Instagram

Kwa kutumia njia hii na kuhakikishia utaweza kuanza kuona like zikiongezeka kwenye post zako na utaweza kuwafikiwa watu wengi zaidi kwa haraka na kwa urahisi. Kitu cha muhimu kumbuka unatakiwa kutumia hashtag ambazo hazizidi 15 na pia hakikisha unatumia hashtag tofauti kwenye kila picha ili kusaidia kufikia watu tofauti kila siku.

Tumia Kamera ya Simu Kama WebCam ya Kompyuta

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.