Mtandao wa TikTok ni moja ya mtandao ambao hivi sasa umeanza kutumiwa na watu wengi zaidi hasa hapa Tanzania. Kutokana na hio watu wengi zaidi wamekuwa wakItumia mtandao huo kuweka video mbalimbali ambazo zimeonekana kufurahisha watu.
Wakati tukiwa bado tuna andaa makala ya jinsi ya kutumia mtandao wa TikTok mwanzo hadi mwisho, hebu leo tuanze na maujanja haya ambayo unaweza kutumia kupakua video zote zilizopo kwenye mtandao wa TikTok bila video hizo kuwa na alama ya username ya mwenye video pamoja na logo yake. Basi unaweza kuangalia Maujanja Dakika Moja na utaweza kujifunza njia hiyo.
LINK MAALUM
Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, video hiyo baada ya kudownload haina alama kwenye kona yenye logo ya TikTok pamoja na username. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unatembelea channel yetu ya YouTube kwani tumeanzisha kipengele kipya cha maujanja dakika ambapo utaweza kujifunza kwa haraka zaidi. Hakikisha una subscribe kuanza kujifunza leo.
habari za asubuhi naomba kuuliza hivi Airtel master card au m pesa master card zinauwezo wa kupokea pesa mtandaoni kama vile amazon paypal na google play store?
Kwa sasa sijajua kama zinao uwezo huo