in

Gazeti App : Soma Habari Zote Tanzania Bila Matangazo

Soma habari, burudika, angalia TV, Tafuta Ajira, Pakua muziki na mengine mengi

Gazeti App : Soma Habari Zote Tanzania Bila Matangazo1:40

Kupata habari imekuwa ni rahisi sana siku hizi, hii inatokana na kuwepo kwa vyanzo vingi vya habari kiasi kwamba ni lazima utaweza kupata habari kupitia vyanzo hivyo. Lakini wote tunajua ni ngumu sana kupata habari kwa ukamilifu kwa kuwa haiwezekani kutembelea tovuti zote hizo kwa pamoja ndio maana tunakuletea App ya Gazeti.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Gazeti ni App itakayokupa uwezo wa kusoma Magazeti ya leo pamoja na habari mbalimbali kwa urahisi kutoka tovuti mbalimbali bila Matangazo, Mbali na tovuti app ya Gazeti inakupa uwezo wa kusikiliza radio pamoja na idhaa za kiswahili kutoka nchi mbalimbali.

Gazeti App pia inakupa urahisi wa kuangalia TV mbalimbali za hapa nchini Tanzania na nje ya nchi kwa urahisi na haraka. Kifupi ni kwamba, Gazeti App inakupa habari zote za Ndani ya Tanzania kwa haraka na kwa urahisi na bila kuwepo kwa Matangazo yoyote au usumbufu wa aina yoyote ile. baadhi ya sifa za app hii ni pamoja na

  • Unaweza kusoma Habari Kutoka Tovuti kubwa za Habari Tanzania.
  • Unaweza Kuangalia TV Mbalimbali za Habari na Burudani kutoka Vyanzo vikubwa.
  • Unaweza kusikiliza Radio za ndani na nje ya Tanzania.
  • Unaweza kusikiliza na kudownload nyimbo mpya za Tanzania kwa haraka na urahisi.
  • Unaweza kuangalia na kupakua filamu kutoka ndani na nje ya Tanzania.
  • Unaweza kuangalia nafasi mpya za ajira kutoka vyanzo vikubwa vya habari Tanzania.
  • Unaweza kufuatilia maswala ya elimu kwa haraka na urahisi
  • Unaweza kufuatilia maswala ya teknolojia.
  • Unaweza kusoma habari za kimataifa.
  • Na mengine mengi…

Kumbuka yote hayo hapo juu na mengine mengi yanapatikana bila matangazo ndani ya App ya Gazeti. Jaribu app ya Gazeti hapo chini, usisahau kutoa maoni yako juu ya vyanzo gani tuongeze au umeonaje app hii kwa ujumla..

Gazeti App : Soma Habari Zote Tanzania Bila Matangazo
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi Hapa Browser Bora Zenye Mfumo wa Akili Bandia (AI)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.