X-TOK : Biashara Zitaendaje Endapo Internet Itazimika.?

Jiunge kwenye mjadala huu kupitia X-TOK tarehe 7/12/2019
X-TOK : Biashara Zitaendaje Endapo Internet Itazimika.? X-TOK : Biashara Zitaendaje Endapo Internet Itazimika.?

Tangu kuingia kwa Internet Tanzania na Dunia nzima, Biashara nyingi zimepata namna ya kujitangaza kwa kufikia wateja wao kwa urahisi, pia biashara mpya zimejitokeza kama wauzaji wa bidhaa mbali mbali wasio na maduka bali huuza kupitia njia ya mtandao. Kampuni za simu, Kampuni za mawasiliano, Bloggers ni moja ya mifano ya kampuni zilizofaidika kutokana na Internet.

X-TOK : Biashara Zitaendaje Endapo Internet Itazimika.?

Kwa upande mwingine zipo kampuni zilizo pitia kipindi kigumu kutokana na mabadiliko ya teknolojia kama magazeti, kampuni za matangazo ya mabango na kampuni nyingine nyingi.

Advertisement

Infinix Mobile Tanzania Kupitia X-TOK EVENT wameandaa mjadala mfupi kuhusu mada hii, “WHAT IS THE FUTURE OF BUSINESS IF THE INTERNET BECOMES OBSOLETE?”

Mjadala Huu utaendeshwa siku ya Jumamosi, tarehe 7 ya mwezi Disemba katika ofisi za Sahara Ventures zilizopo barabara ya Bagamoyo Rd, Jengo la Bayport ghorofa ya 6, kuanzia saa 4 na nusu asubuhi mpaka saa 8 mchana. Ili kujiunga na mjadala huu unaweza jisajili Hapa.

X-TOK : Biashara Zitaendaje Endapo Internet Itazimika.?

Kutakuwa na wageni maalum ambao ni pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano Princel H Glorious, Founder wa Ona Stories. Ndugu Cynthia Bavo ambaye ni C.E.O na Founder wa MyJobPass na Ndugu Anthony Luvanda ambaye ni Mjasiriamali pamoja na Public Speaker.

Kuhusu XTOK

XTOK ni event ambayo huandaliwa na kampuni ya simu, Infinix Mobile Tanzania kwa lengo la kuwakutanisha vijana wapenda teknolojia, ubunifu na trends mbali mbali ili kujadiliana kwa lengo la kutafuta suluhisho. Hii ni imara ya 5 kufanyika kwa event hii.

3 comments
  1. Asante kwa kutusaidia ila ningependa kujua je utanisaidiaje Mimi ambaye nataka kujifunza zaid mambo yateknolojia ilikuwa nauwezo mkubwa wakufanya biashara yangu kupitia mtandao? Unaweza wasiliana zaid kwa 0768380537

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use