Jiandae na Simu Mpya za Samsung Galaxy A30s na Galaxy M20s

Samsung kuja na maboresho ya simu za Galaxy A30 na Galaxy M20
Jiandae na Simu Mpya za Samsung Galaxy A30s na Galaxy M20s Jiandae na Simu Mpya za Samsung Galaxy A30s na Galaxy M20s

Kampuni ya Samsung mwaka huu 2019 ilitangaza kuachana na simu za Samsung Galaxy J na badala yake kampuni hiyo iliangazia zaidi simu mpya za Galaxy A pamoja na matoleo mpya ya simu za Galaxy M.

Hadi sasa zipo simu nyingi za bei nafuu kutoka Samsung ambazo zinatumia majina ya Galaxy A huku moja ya simu hizi ikiwa ni Galaxy A30 ambayo imezinduliwa mapema mwezi wa tatu mwaka huu 2019. Vilevile kwa upande wa Galaxy M20 Samsung ilizindua simu hii mwezi wa pili mwaka huu ikiwa ni moja ya matoleo ya awali ya simu mpya za Galaxy M.

Sasa hivi karibuni kwa mujibu wa tovuti ya 91Mobile, Samsung inataraji kuja na simu mpya ya Galaxy A30s ambayo inatarajiwa kuwa na maboresho machache ikiwa pamoja na kamera tatu kwa nyuma tofauti na toleo la sasa la Galaxy A30. Vilevile simu hiyo mpya ya Galaxy A30s pia inatarajiwa kuwa na RAM kubwa zaidi huku pia ikiwa na chaguo la RAM ya GB 3.

Advertisement

Jiandae na Simu Mpya za Samsung Galaxy A30s na Galaxy M20s

Vilevile kwa mujibu wa tovuti ya Galaxy Club, kampuni ya Samsung pia inasemekana kujiandaa na toleo jipya la Samsung Galaxy M20s toleo ambalo linasemekana kuja na maboresho zaidi kama vile battery kubwa zaidi ya 5,830 mAh, tofauti na Galaxy M20 ambayo yenyewe inakuja na battery ya 5,000 mAh.

Jiandae na Simu Mpya za Samsung Galaxy A30s na Galaxy M20s

Kwa sasa tayari model number za simu hizi zimesha julikana, huku Galaxy M20s ikiwa imepewa Model number ya SM-M207 na Galaxy A30s ikiwa imepewa Model Number ya SM-A307FN. Simu hizi zinasemekana kutoka mwaka huu huku Galaxy A30s ikiwa ndio simu itakayo tangulia kutoka ikikadiriwa kutoka ndani ya mwezi wa nane au mwezi wa tisa.

Kwa sasa bado hakuna ripoti kamili kuhusu sifa kamili za simu hizi, kama kutakuwa na taarifa yoyote kuhusu simu hizi hakika utakuwa wa kwanza kuipata kwa kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku. Kwa habari zaidi hakikisha unatembelea channel yetu ya Tanzania Tech Hapa.

1 comments
  1. nadhani samsung wamedhamiria kuchukua soko la simu zao hizi kuwapiku tecno infinix nk ni muda wa haya makampuni kujipanga soko lao lisibebwe na samsung but samsung nao simu zao poa nlikuwa tecno now nimehamia kwao na A20 ni bomba

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use