Kampuni ya Samsung Yatangaza Kuachana na Simu za Galaxy J

Sasa simu za Galaxy J zitakuwa zinatoka kwa majina ya Galaxy A
Kampuni ya Samsung Yatangaza Kuachana na Simu za Galaxy J Kampuni ya Samsung Yatangaza Kuachana na Simu za Galaxy J

Kama wewe ni mfuatiliaji wa maswala ya simu hasa za Samsung basi utakuwa unakua kuwa Samsung haijazindua simu yoyote mpya ya Galaxy J mwaka huu, lakini pia kama uko makini utakuwa umegundua hadi sasa mwaka huu samsung imezindua simu nyingi za Galaxy A.

Pengine hiyo ilikuwa ni moja ya ishara ya kuonyesha Samsung imeamua kuweka macho yake zaidi kwenye simu za Galaxy A na kuamua kuachana na matoleo ya simu za Galaxy J. Kupitia video ambayo imetoleo kwa ajili ya simu ya Galaxy A50, Samsung inaonekana kutangaza kuachana na simu za Galaxy J na sasa simu hizo zitakuwa kwa majina ya Galaxy A.

Advertisement

Simu zote mpya za Galaxy A zinakuja zikiwa zimeboreshwa zaidi huku zikiwa zinakuja na kamera mbili kwa nyuma pamoja na vioo vikubwa, mbali na hayo pia simu hizo zinapatikana kwa bei nafuu. Hata hivyo simu za Galaxy A zinakuja na sifa bora zaidi huku zikiwa na muonekano bora kuliko simu za zamani za Galaxy J.

Kwa sasa tunasubiri simu mpya ya Galaxy A90 au Galaxy A80 ambayo inasemekana kuja na kamera bora ambayo itakuwa ni ya ku-slide pamoja na muonekano wa kisasa. Simu hii pia inasemekana kuzinduliwa rasmi siku ya kesho kwenye mkutano maalum wa uzinduzi wa simu mpya za Galaxy A, ambapo tunategemea kuona simu nyingi mpya za daraja la kati kutoka Samsung.

Kampuni ya Samsung Yatangaza Kuachana na Simu za Galaxy J

Kujua yote kuhusu simu hizi mpya za Galaxy A, endelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kwani tutakuwa mubashara kabisa kwenye uzinduzi wa simu hizo mpya za Galaxy A hapo siku ya kesho.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use