Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A10s

Zifahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy A10s
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A10s Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A10s

Baada ya kampuni ya Samsung kuzindua simu mpya ya Galaxy A10 mapema mwezi wa tatu mwaka huu, hatimaye hivi leo samsung imerudi tena na Galaxy A10s toleo jingine la simu hiyo ya bei nafuu kutoka Samsung.

Galaxy A10s imefanyiwa maboresho na sasa inakuja na battery kubwa zaidi, kamera mbili kwa nyuma pamoja na sehemu ya fingerprint. Simu hii pia inasemekana kuja ikiwa bora zaidi hasa upande wa kamera za nyuma ambazo sasa zinakuja na Megapixel 13 pamoja na Megapixel 2.

Sifa za Samsung Galaxy A10s

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A10s

Advertisement

Vilevile Galaxy A10s sasa inakuja na sehemu ya Fingerprint ambayo inapatikana kwa nyuma ya simu hiyo tofauti na Galaxy A10 ambayo yenyewe haina sehemu ya fingerprint. Mabadiliko mengine ni battery ya simu hii ambapo sasa A10s inakuja na battery kubwa ya 4000 mAh ambayo inasemekana kudumu na chaji zaidi.

Bei ya Samsung Galaxy A10s

Kwa mujibu wa Samsung, hadi sasa bado bei haija tangazwa rasmi, ila tegemea kuipata simu hii kwa bei ya makadirio kati ya shilingi za kitanzania Tsh 390,000 hadi Tsh 450,000. Kumbuka bei hii ni kwa makadirio hivyo bei inaweza kubadilika pale bei halisi itakapo Tangazwa. Kwa habari zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech.

4 comments
  1. Naomba kujua bei ya samsung galaxy a10s halisi mnayoiuza hyo simu.Nimeipenda naiitaji kuinunua naomba feedback mapema.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use