in

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya za Honor 20 na 20 Pro

Zifahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya Honor 20 Pro na Honor 20

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya za Honor 20 na 20 Pro

Wakati kampuni ya Huawei ikiendelea kupitia kwenye vikwanzo vya kibiashara vinavyo wekwa na Marekani, hapo jana kampuni hiyo imeonyesha kuwa haijali vikwazo hivyo kwa kuendelea kuzindua simu zake mpya kama ilivyo pangwa.

Kampuni ya Honor ambayo ni sehemu ya kampuni ya Huawei, hapo jana ilizindua simu zake mpya za Honor 20 na Honor 20 Pro, simu ambazo zinakuja na sifa nzuri sana pamoja na muonekano wa kisasa.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Tukianza na Honor 20 Pro, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.26 kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD chenye uwezo wa resolution hadi pixel 1080 x 2340. Kioo hicho kwa mbele kimekatwa na kuruhusu sehemu ya kamera ya mbele ambayo hii inakuja na uwezo wa Megapixel 32, kwa nyuma simu hii inakuja na kamera nne zenye uwezo wa Megapixel 48, Megapixel 16, Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2, zote zikiwa na uwezo wa kurekodi video za 4K.

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya za Honor 20 na 20 Pro

Simu hii inakuja ikiwa inaendeshwa na processor iliyotengenezwa na Huawei, processor ya HiSilicon Kirin 980 ambayo kwenye simu hii ya Honor 20 Pro, inasaidiwa na RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 256. Kwa bahati mbaya ukubwa huu hauwezi kuongezwa kwa namna yoyote kwani simu hii haina sehemu ya kuweka Memory Card.

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya za Honor 20 na 20 Pro

Mbali na hayo yote simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa hadi 4000mAh, battery yenye uwezo wa kudumu na chaji zaidi ya siku moja kulingana na matumizi. Pia Honor 20 Pro inakuja na teknolojia ya Fast Charging ambayo inafanya simu hii kujaa chaji hadi asilimia 50 kwa muda wa nusu saa (dakika 30). Mbali ya hayo sifa nyingine za Honor 20 Pro ni kama zifuatazo.

Sifa za Honor 20 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.26 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~412 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.6 GHz Cortex-A76 & 2×1.92 GHz Cortex-A76 & 4×1.8 GHz Cortex-A55).
  • Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 980 (7 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP10.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 256 ikiwa Haina uwezo wa kuongezewa na Memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 ikiwa na f/2.0, 0.8µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne yenye Megapixel 48, f/1.4, 28mm (wide), 1/2″, 0.8µm, Laser/PDAF, OIS. Nyingine ina Megapixel 16, f/2.2, 13mm (ultrawide), 1/3.1. Nyingine ina Megapixel 8, f/2.4, 80mm (telephoto), 1/4.4″, Laser/PDAF, OIS, 3x optical zoom. Kamera ya mwisho ina Megapixel 2, f/2.4, 27mm (wide), dedicated macro camera.
    Kamera zote hizo zinasaidiwa na HDR, Panorama pamoja na flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 22.5W (50% in 30 min).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.1 Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa mbili za Phantom Blue na Phantom Black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa pembeni).

Bei ya Honor 20 Pro

Kwa upande wa bei, Honor 20 Pro inategemewa kuingia sokoni hivi karibuni na itakuwa inauzwa kwa Euro €600 ambayo hii ni sawa na takribani Shilingi za Kitanzania Tsh 1,540,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Tukiachana na simu hiyo, Honor 20 nayo inakuja na sifa zinasofanana kabisa na sifa za Honor 20 Pro japokuwa kuna tofauti kidogo kwenye upande wa Kamera za nyuma, Uwezo wa battery, Uwezo wa RAM, Rangi pamoja na ukubwa wa ROM, vitu vingine vyote vinafanana. Ili kujua tofauti ya Honor 20 na Honor 20 Pro ni vyema pia kufahamu sifa za Honor 20.

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya za Honor 20 na 20 Pro

Sifa za Honor 20

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.26 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~412 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.6 GHz Cortex-A76 & 2×1.92 GHz Cortex-A76 & 4×1.8 GHz Cortex-A55).
  • Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 980 (7 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP10.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa Haina uwezo wa kuongezewa na Memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 ikiwa na f/2.0, 0.8µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne yenye Megapixel 48, f/1.4, 28mm (wide), 1/2″, 0.8µm, Laser/PDAF, OIS. Nyingine ina Megapixel 16, f/2.2, 13mm (ultrawide), 1/3.1. Nyingine ina Megapixel 2, f/2.4, 80mm (telephoto), 1/4.4″, Laser/PDAF, OIS, 3x optical zoom. Kamera ya mwisho ina Megapixel 2, f/2.4, 27mm (wide), dedicated macro camera.
    Kamera zote hizo zinasaidiwa na HDR, Panorama pamoja na flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3750 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 22.5W (50% in 30 min).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.1 Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa tatu za Midnight Black, Sapphire Blue na Icelandic white.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa pembeni).

Bei ya Honor 20

Kwa mujibu wa tovuti ya Honor, simu hii ya Honor 20 inategemewa kutoka siku za karibuni na bei yake itakuwa kati ya Euro €500 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania Tsh 1,283,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kutokana na kupanda au kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya za Honor 20 na 20 Pro
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.