Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy M40 Mwezi June 11

Baada ya ukimya, sasa jiandae na simu mpya ya Galaxy M40
Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy M40 Mwezi June 11 Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy M40 Mwezi June 11

Kampuni ya Samsung imekuwa kimya kidogo lakini ukimya huo unategemewa kuvunjika tarehe 11 mwezi ujao wa sita mwaka huu 2019.

Kwa mujibu wa tovuti ya 91mobiles, Samsung inatarajia kuzindua simu mpya ya Galaxy M40, simu ambayo inasemekana kuja na sifa nzuri pamoja na muonekano wa kisasa. Kwa mujibu wa tovuti hiyo simu hiyo inakuja na kioo cha Infinity-O display chenye kamera ya mbele ambayo iko kwenye kioo.

Advertisement

Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy M40 Mwezi June 11

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu ambazo zinasemekana kuwa na uwezo wa Megapixel 32, Megapixel 8 na Megapixel 5. Kamera zote zinauwezo wa kuchuku video za 4k, huku pia zikiwa zinasaidiwa na Flash ya LED.

Mbali na hayo simu hii inasemekana kuja na processor ya Snapdragon 675 SoC ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 128, ukubwa huo unaweza kuongezwa na memory card ya hadi TB 1.

Kwa upande wa mfumo, simu hii inasemekana kuendeshwa na mfumo wa Android 9 Pie, huku juu yake ikiwa na mfumo wa Samsung wa One UI. Vilevile simu hii inakuja na battery kubwa ya 5000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.

Simu hii inasemekana kuanza kupatikana mwezi ujao nchini India kwa rupee ya india INR 20,000 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 658,000 bila kodi. Simu hii inategemewa kupatikana maususi kupitia kwenye soko la mtandaoni la Amazon la nchini India.

Kama unataka kujua sifa kamili za simu hii pamoja na bei hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tutakupa habari hizo pindi simu hii itakapo tangazwa rasmi. Kama unapenda maujanja hakikisha una subscribe kwenye channel yetu ili kujifunza kwa vitendo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use