in

Huawei Yaruhusiwa Kutumia Mfumo wa Android kwa Miezi Mitatu

Watumiaji wa simu za Huawei kutegemea kupata masasisho hivi karibuni

Huawei Yaruhusiwa Kutumia Mfumo wa Android kwa Miezi Mitatu

Baada ya sakata la kampuni ya Huawei hapo jana kusitishiwa huduma zake na baadhi ya makampuni ya nchini Marekani ikiwepo kampuni ya Google ambayo inamiliki mfumo wa Android, hivi leo habari mpya zinasema kuwa Huawei imeruhusiwa kuendelea kutumia mfumo wa Android kama kawaida kwa muda wa miezi mitatu.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, Huawei imepewa leseni maalum ambayo inaruhusu kampuni hiyo kuendelea kutumia mfumo huo kama kawaida bila masharti ya kukosa baadhi ya huduma za Google.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Leseni hiyo ambayo imetolewa na Idara ya Biashara ya Marekani kwa kampuni ya Huawei, inaruhusu kampuni hiyo kutuma sasisho kwenye simu za Huawei ambazo tayari ziko sokoni au ambazo zimeingia sokoni kabla ya tarehe 16 May 2019. Hata hivyo, leseni hiyo pia inaruhusu kampuni hiyo kuendelea na kuboresha vifaa vyake vya kimawasiliano na kuweza kutuma sasisho la ulinzi kwenye vifaa hivyo.

Huawei Yaruhusiwa Kutumia Mfumo wa Android kwa Miezi Mitatu

Hata hivyo, leseni hiyo ambayo inasemekana kuisha tarehe 19 August 2019, pale itakapo fikia ukomo wake Huawei haita ruhusiwa kutumia mfumo wa Android kama, bali sasa itaruhusiwa kutumia mfumo huo bila huduma za muhimu za Google kama vile, Google Maps, Play Store, YouTube, Chrome, Gmail pamoja na huduma nyingine nyingi ambazo zinafanya mfumo huo uweze kufanya kazi kwa usahihi.

Kwa sasa inasemekana kuwa Huawei inategemea kuja na mfumo wake ambao ulianza kufanyiwa kazi na Huawei hapo mwaka jana 2018 kwa kuhofia hatua kama hii. Mbali na hayo pia huawei inasemekana kuja na chip au processor zake kwa ajili ya laptop zake za Matebook ambazo zinatumia chip kutoka kampuni ya Intel, kampuni ambayo nayo pia imesitisha kutoa huduma kwa kampuni ya Huawei.

Huawei Yaruhusiwa Kutumia Mfumo wa Android kwa Miezi Mitatu
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.