in

Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 3a na Pixel 3a XL

Hizi hapa sifa kamili pamoja na bei ya simu mpya za Google Pixel 3a na Pixel 3a XL

Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 3a na Pixel 3a XL

Kampuni ya Google hapo jana kupitia mkutano wa Google I/O 2019 imetangaza ujio wa simu zake mpya za Google Pixel 3a na Google Pixel 3a XL. Simu hizi ni moja kati ya simu ambazo zipo kwenye list ya simu ambazo zinatarajiwa kutoka kwa mwezi wa tano mwaka 2019.

Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 3a na Pixel 3a XL

Kwa upande wa sifa, simu hizi zinakuja zikiwa na sifa za kawaida tofauti kidogo na simu za mwaka jana (2018) za Google Pixel 3 na Pixel 3 XL. Tukianza na simu mpya ya Pixel 3a, yenyewe inakuja na kioo cha OLED chenye ukubwa wa inch 5.6 ambacho pia kinakuja na resolution ya pixel 1080 x 2220 huku kioo hicho kikiwa kina ulinzi wa Dragontrail protection.

Kwa mbele ya simu hiyo kuna kamera ya Megapixel 8 yenye uwezo wa kuchukua video za 1080p pamoja na teknolojia ya HDR, Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera moja ya Megapixel 12 iliyo boreshwa kwa software pamoja na teknolojia mbalimbali kutoka kampuni ya Google.

Simu hii inaendeshwa na processor ya Snapdragon 670 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64. Pixel 3a na Pixel 3a XL zote hazina sehemu ya memory card hivyo hutoweza kuongeza ukubwa huo wa ndani. Sifa nyingine za Pixel 3a ni kama zifuatazo.

Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 3a na Pixel 3a XL

Sifa za Google Pixel 3a

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.6 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~441 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.0 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM670 Snapdragon 670 (10 nm) Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 615.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 zote zikiwa Hazina uwezo wa kuongezewa na memory card.
 • Ukubwa wa RAM – RAM GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 ikiwa na f/1.8, 28mm (wide).
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 12.2 yenye f/1.8, 28mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, OIS, dual pixel PDAF. Huku ikiwa inasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1 Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa tatu za Clearly White, Just Black na Not Pink.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM, Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Bei ya Google Pixel 3a

Kwa upande wa bei, Pixel 3a inapatikana sasa kwa dollar za marekani $399 sawa na takribani Shilingi za kitanzania Tsh 919,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 3a na Pixel 3a XL

Kwa upande wa simu mpya ya Google Pixel 3a XL, yenyewe inakuja ikiwa na sifa zinazo fanana na Google Pixel 3a lakini tofauti yake kubwa ni ukubwa wa kioo. Pixel 3a XL inakuja na kioo cha OLED chenye inch 6.0 ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2160 pixels. Sifa nyingine za Simu hii zinafanana sana na Google Pixel 3a XL, kujua zaidi hizi hapa ndio sifa kamili za Pixel 3a XL.

Sifa za Google Pixel 3a XL

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~402 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.0 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM670 Snapdragon 670 (10 nm) Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 615.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 zote zikiwa Hazina uwezo wa kuongezewa na memory card.
 • Ukubwa wa RAM – RAM GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 ikiwa na f/1.8, 28mm (wide).
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 12.2 yenye f/1.8, 28mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, OIS, dual pixel PDAF. Huku ikiwa inasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3700 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1 Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa tatu za Clearly White, Just Black na Not Pink.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM, Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Dalili za Ugonjwa wa Kupenda Smartphone Kupita Kiasi

Bei ya Google Pixel 3a XL

Kwa upande wa bei, Pixel 3a XL inapatikana sasa kwa dollar za marekani $479 sawa na takribani Shilingi za kitanzania Tsh 1,103,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.