in

Jiandae na Smartphone Hizi Mpya Mwezi Huu wa Tano (2019)

Simu Hizi ni pamoja na Honor 20, OnePlus 7 pamoja na Google Pixel 3a

Jiandae na Smartphone Hizi Mpya Mwezi Huu wa Tano (2019)

Simu mpya zinatoka kila mwezi kiasi kwamba ni ngumu kujua kila simu ambayo inatoka kila mwezi, hadi kufikia sasa tayari simu nyingi sana zimetoka na nyingine nyingi zinatarajiwa kutoka mwezi huu wa tano.

Kupitia makala hii utaweza kujua baadhi ya simu mpya ambazo zinatarajiwa kutoka mwezi huu wa tano ikiwa pamoja na baadhi ya sifa za simu hizi. Kumbuka kuwa simu hizi bado hazijatoka rasmi ila unaweza kupata sifa za simu hizo kwa kubofya link kwenye jina la simu husika. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie simu hizi.

OnePlus 7 na OnePlus 7 Pro

Jiandae na Smartphone Hizi Mpya Mwezi Huu wa Tano (2019)

Hivi karibuni tetesi zimeibuka mtandaoni ambapo tayari inasemekana sifa za simu hizi zimesha julikana rasmi huku kampuni ya OnePlus ikitarajia kuzindua simu hizi mpya mwezi huu wa tano tarehe 14. Kwa mujibu wa tetesi, simu hizi zinatarajiwa kuja na kamera tatu za nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 48.

Usinunue Simu ya Android au iPhone ya Zamani

Mbali na hayo inasemekna kuwa simu hii itakuja bila ukingo wa juu na itakuwa haina kamera ya mbele iliyoko kwenye kioo bali inasemekana kuwa na kamera inayotumia mota inayotoka kwa nyuma kama inavyo onekana hapa juu.

Google Pixel 3a na Google Pixel 3a XL

Jiandae na Smartphone Hizi Mpya Mwezi Huu wa Tano (2019)

Google inatarajia kuingiza sokoni toleo jipya la bei rahisi la simu ya Google Pixel 3, Simu hii awali ilikuwa inajulikana kama Pixel 3 Lite lakini kwa sasa inajulika kama Pixel 3a. Kwa mujibu wa tetesi za mtandaoni, Pixel 3a inatarajiwa kuja na processor ya Snapdragon 710 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 au GB 128.

Mbali na hayo simu hii pia inatarajiwa kuja na kamera ya Megapixel 12.2 yenye sifa mbalimbali kama vile Night Sight, Motion Focus na Portrait Mode ambazo zote zinafanya kamera hiyo kuwa na nguvu sana kuliko idadi ya Megapixel zake. Kwa mbele simu hii inatarajiwa kuja na kamera ya Megapixel 8 yenye uwezo wa kurekodi video za 1080p.

Kampuni ya Nokia Kubadilisha Logo Yake ya "NOKIA"

Honor 20 na Honor 20 Pro

Jiandae na Smartphone Hizi Mpya Mwezi Huu wa Tano (2019)

Kampuni ya Huawei inatarajia kuja na simu mpya ya Honor 20 na Honor 20 Pro, simu hizi zinatarajiwa kutoka mwezi huu tarehe 21. Kwa mujibu wa tetesi Honor 20 inatarajiwa kuja na kamera tatu kwa nyuma na kama ilivyo OnePlus 7 nayo pia inakuja MP 48.

Mbali na hayo Honor 20 Pro inasemekana kuwa na kamera nne japo kuwa hilo halina uhakikisa sana. Mbali na hayo simu hizi zinatarajiwa kuwa na processor yenye nguvu ya Kirin 980 ambayo inasaidiwa na RAM ya kati ya GB 6 au GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 256.

Na hizo ndio simu chache ambazo zinategemewa kuja mwezi huu wa tano, kumbuka simu nyingine zinaweza kutoka ndani ya mwezi huu hivyo hakikisha unatembelea Tanzania Tech ili kujua sifa kamili pamoja na bei ya simu zote zitakazo toka.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.