in

Jinsi ya Kuzuia Kikamilifu Apps Ku-update Zenyewe Kupitia Play Store

Tumia njia hizi ili kuweza kuzima kikamilifu update za Apps mbalimbali kupitia Play Store

Jinsi ya Kuzuia Kikamilifu Apps Ku-update Zenyewe Kupitia Play Store

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android basi ni lazima unajua kuwa, kuna wakati apps ambazo ume install kwenye simu yako zinaji update zenyewe bila hata wewe kuruhusu, mara nyingi hii ni tatizo hasa kwa watu ambao unakuta wana MB chache kwenye simu na wanataka kufanya vitu mbalimbali tofauti na ku-update apps hizo.

Sasa kuliona hili leo tumekuletea njia ya usahihi ya kuweza kuzima (Auto Update) kupitia simu yako ya mkononi ya Android, njia ambayo haifanani na ile njia ya kuzima update za apps zote kupitia sehemu ya settings kupitia soko la Play Store. Kama kwa namna yoyote unataka kutumia njia ya settings unaweza kuipata kupitia settings kwenye soko la Play Store.

Jinsi ya Kuzuia Kikamilifu Apps Ku-update Zenyewe Kupitia Play Store

Lakini kumbuka, mara nyingi njia hii huwa haifanyi kazi na unaweza kuona apps zako bado zina endelea kuji update zenyewe pale tu unapowasha internet. Sasa kama ikitokea hivyo nakushauri kufuata njia hizi ambazo na uhakikika kwa asilimia 100 zitakusaidia kuzima Auto Update za apps mbalimbali ndani ya simu yako.

Uzuri wa njia hii ni kuwa utaendelea kupokea meseji za kukujulisha kwa unatakiwa ku-update lakini apps hizo hazitoweza kuji-update zenyewe hadi hapo wewe utakapo ruhusu. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia hizi.

Kwa kuanza ingia kwenye soko la Play Store kisha nenda kwenye app ambayo unataka kuzuia updates, kisha bofya vimishale vitatu vilivyoko juu upande wa kulia kisha utaona sehemu imeandikwa Enable auto update, ondoa tiki kwenye sehemu hiyo na utakuwa umemaliza. Rudia hatua hii kwenye kila app ambayo hutaki ijiupdate yenyewe.

Jinsi ya Kuzuia Kikamilifu Apps Ku-update Zenyewe Kupitia Play Store

Natumaini makala hii fupi itakusaidia kuweza kuzima Auto Updates kwenye apps mbalimbali kupitia soko la Play Store. Kumbuka unaweza kutumia njia zote mbili ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi kulingana na mahitaji yako.

Kwa maujanja zaidi hakikisha una Subscribe kwenye channel yetu ili kuweza kifunza maujanja kama haya kwa vitendo. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.

Tofauti ya Battery za Simu Zenye Teknolojia ya Li-ion na Li-Po

Written by Jackline John

Jack ni mpenzi wa teknolojia napenda kuandika kuhusu maujanja, simu na kompyuta. Unaweza kunipa maujanja kupitia [email protected]

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments