in

Galaxy A2 Core Simu Mpya ya Bei Rahisi Kutoka Samsung

Zifahamu kwa undani hizi hapa sifa na bei ya Samsung Galaxy A2 Core

Galaxy A2 Core Simu Mpya ya Bei Rahisi Kutoka Samsung

Mwaka jana (2018) kampuni ya Samsung ilizindua Galaxy J2 Core simu ya kwanza yenye kutumia mfumo wa Android Go. Kama unavyojua mfumo wa Android Go ni mfumo ambao unatambulika kuwepo kwenye simu za Android zenye uwezo wa RAM chini ya GB 1.

Sasa kwa sababu Samsung imetangaza kuachana na simu za Galaxy J, mwaka huu Samsung imekuja na toleo la pili la simu hii toleo ambalo limepewa jina la Galaxy A2 Core. Kama ilivyo Galaxy J2 Core simu hii pia inakuja na mfumo wa Android Go ambao unafanya simu hii kuwa na RAM ya GB 1.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sifa nyingine za simu hii ni pamoja kioo cha inch 5.0 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD huku kikiwa kina uwezo wa resolution hadi 540 x 960 pixels. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Selfie ya megapixel 5 yenye uwezo wa f/2.2 huku kwa nyuma pia ikiwa inakuja na kamera ya Megapixel 5 yenye uwezo wa kurekodi video za 1080p@30.

Simu hii inakuja na processor ya Exynos 7870 Octa ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 1 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 16 au GB 8, unaweza kuongeza ukubwa huo kwa kutumia sehemu ya memory card ambayo inapokea MicroSD Card yenye uwezo wa hadi GB 256. Sifa nyingine za Galaxy A2 Core ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A2 Core

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.0 chenye teknolojia ya HD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 540 x 960 pixels, na uwiano wa 116:9 ratio (~220 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie Go)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.6 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7870 Quad Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-T830.
  • Ukubwa wa Ndani – Zipo simu mbili moja ikiwa na GB 8 na nyingine ikiwa na GB 16 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM –  RAM ya GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 5 yenye HDR, panorama na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery Inayotoka ya Li-Ion 2600 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Blue
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Accelerometer na proximity.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Bei ya Samsung Galaxy A2 Core

Kwa mujibu wa tovuti ya fonearena, simu hii inatarajiwa kuanza kupatikana kwa nchini India kwa rupee ya India INR 5,300 ambayo ni sawa na Tsh 177,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Galaxy A2 Core Simu Mpya ya Bei Rahisi Kutoka Samsung
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.