in

Video : Simu Inayo jikunja ya Xiaomi Yaonekana kwenye Video

Hii ndio simu ya kwanza ya Xiaomi inayojikunja

Simu kutoka Xiaomi inayojikunja

Kama nilivyo kwambia mwaka 2019 utakuwa ni mwaka wa simu zinazo jikunja na hili sio geni kwako kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania tech. Lakini kama ni mara ya kwanza unajiunga nasi basi labda nikwambie kuwa mwaka huu tegemea kuona teknolojia za simu zinazo jikunja kutoka makampuni mbalimbali ya utengenezaji wa simu.

Kutokea Samsung ilipo tangaza ujio wa simu yake inayo jikunja, kampuni nyingine za simu nazo zimeonyesha nia ya dhati ya kuzindua simu ambazo pia zitakuwa zinajikunja kama simu hiyo mpya ya Samsung Galaxy F.

Baadhi ya makampuni ambazo zimeonyesha nia hiyo ni pamoja na kampuni ya LG, Huawei, Motorola pamoja na kampuni ya Xiaomi ambayo hivi leo imeonyesha mfano wa simu yake inayojikunja kupitia video iliyotokea kwenye mtandao wa Weibo, ambayo inaonyesha mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo ya Xiaomi Lin Bin, akitumia simu hiyo ambayo hadi sasa bado hakuna taarifa ya ujio wake.

Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, simu hiyo inaonekana kujikunja penda mbili za kushoto na kulia huku pia ikionekana sehemu ya kuzima na kuwasha ikiwa ipo kwa juu ya simu hiyo. Vilevile kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, simu hiyo inasemekana inakuja na kioo chenye uwiano wa 3:2.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Anyway kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi za ujio wa simu hii kutoka Xiaomi, lakini huenda mwaka huu kampuni hii ikaja na simu hii ikitegemea kuwa kampuni ya Xiaomi sasa imejikita katika ugunduzi wa teknolojia mpya mbalimbali za simu ikiwa pamoja na teknolojia ya mpya ya Fingerprint iliyo onyeshwa na Xiaomi hivi karibuni.

Kwa taarifa zaidi kuhusu simu hii pamoja na mengine mengi kuhusu teknolojia pamoja na kampuni ya Xiaomi, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.