in

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Hizi hapa ndio laptop 15 zilizofanya vizuri kwa mwaka 2018

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Mwaka 2018 una karibia mwishoni na kwenye kipindi hichi ni wakati mzuri sana wa kuangalia list ya laptop bora za mwaka 2018. Kama wewe ni mfuatiliaji wa maswala ya teknolojia najua utakuwa unajua mwaka 2018 sio mwaka wa laptop sana kwani tumeona macho ya watu wengi sana yakielekezwa kwenye ulimwengu wa Smartphone zaidi kuliko laptop.

Lakini pamoja na hayo ziko laptop mpya mbalimbali ambazo zimetoka mwaka huu 2018 na kufanikiwa kuingia kwenye list hii ya laptop bora za mwaka 2018. Hivyo basi kama ulikuwa unatafuta laptop bora ya kuanza nayo mwaka 2019 pengine hii ni makala sahihi sana kwako, basi bila kupoteza muda twende tukangalie laptop hizi bora.

15. Samsung Notebook 9

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kama wewe ni mpenzi wa laptop za Macbook Pro lakini huna pesa ya kutoka basi laptop ya Samsung Notebook 9 ni laptop nzuri sana kwako. Mbali ya kuwa ni laptop nzuri lapo hii inakuja na sifa nzuri sana ambazo ukweli zinatosha kwa kila mtumiaji wa kawaida wa laptop.

Sifa za Laptop ya Samsung Notebook 9

 • CPU: Intel i7-8550U
 • Graphics: Nvidia GeForce MX150
 • RAM: 8GB-16GB
 • Screen: 15-inch 1,920 x 1,080 LED
 • Storage: 256-512GB SSD

14. Acer Swift 3

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kama ulikuwa unatafuta laptop nzuri kwa bei nafuu basi Acer Swift 3 ni moja kati ya laptop nzuri sana kuwa nayo. Laptop hii kama ilivyo Notebook 9 laptop hii pia inakuja na uwezo mzuri sana na pia inasemekana bei yake ni rahisi zaidi.

Sifa za Laptop ya Acer Swift 3

 • CPU: Dual-core Intel Core i3 – i7
 • Graphics: Intel HD Graphics 620
 • RAM: 4GB – 8GB DDR4
 • Screen: 14-inch full HD (1920 x 1080) ComfyView IPS
 • Storage: 128GB – 256GB SSD

13. Google Pixelbook

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kutumia programu za Android basi laptop hii ni bora sana kwako. Laptop hii ya Google Pixelbook inakuja na uwezo mzuri sana pamoja na uwezo wa kipekee wa kutumia programu za mfumo wa Android. Pia laptop hii ina kioo chenye uwezo wa touchscreen.

Sifa za Laptop ya Google Pixelbook

 • CPU: Intel Core i5 – i7
 • Graphics: Intel HD Graphics 615
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 12.3-inch QHD (2,400 x 1,600) LCD touchscreen
 • Storage: 128GB – 512GB SSD

12. Apple MacBook 12-inch (2017)

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Japo kuwa MacBook 12-inch (2017) ni laptop ya mwaka jana lakini bado laptop hii iko kwenye chat ya laptop bora kwa mwaka 2018. Kwa mtu yoyote anaijua laptop najua lazima atakuwa anajua uwezo wa laptop hii, Laptop hii ina ubora wa kila sekta hivyo kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi hii ndio laptop bora ya kuwa nayo kwa mwaka 2018 – 2019.

Sifa za Laptop ya MacBook 12-inch (2017) 

 • CPU: Intel Core M3 1.2GHz – Intel Core i7 1.4GHz
 • Graphics: Intel HD Graphics 615
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 12-inch, (2,304 x 1,440) IPS 16:10
 • Storage: 256GB – 512GB SSD

11. Acer Switch 3

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kama wewe unatafuta laptop ambayo pia ni tablet basi Acer Switch 3 ni laptop bora sana kuwa nayo. Mbali na yote laptop hii inakuja na uwezo mzuri sana, vile vile Acer Switch 3 inapatikana kwa bei rahisi sana tofauti na laptop nyingine kwenye list hii.

Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020)

Sifa za Laptop ya Acer Switch 3

 • CPU: 1.10GHz Intel Pentium Quad Core N4200 – Intel Core i3 7100U
 • Graphics: Intel HD Graphics 505
 • RAM: 4GB
 • Screen: 12.2-inch, 1920 x 1200 IPS LCD touchscreen
 • Storage: 64GB – 128GB eMMC

10. Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch)

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch) ni laptop nzuri sana kwa ajili ya wanafunzi pamoja na wafanyakazi hasa wabunifu wa michoro mbalimbali. Laptop hii ina uwezo mkubwa sana na ukweli hii ni moja kati ya laptop za 2 in 1 zenye uwezo mkubwa sana. Kama wewe ni unapenda kutumia laptop yenye nguvu na ambayo inaweza kuwa tablet basi Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch) ni laptop bora sana kwaajili yako.

Sifa za Laptop ya Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch)

 • CPU: Intel Core i5-7300U – Intel Core i7-8650U 1.9GHz
 • Graphics: Intel UHD Graphics 620; Nvidia GeForce GTX 1050 (2GB GDDR5 VRAM)
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 3,000 x 2,000 (267 ppi) PixelSense display, 3:2 aspect ratio
 • Storage: 256GB – 1TB SSD

9. Razer Blade 15

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Sababu kubwa kabisa ya Razer Blade 15 kuingia kwenye list hii ni kutoka na ubora wake. Laptop hii ni moja kati ya laptop bora sana kwa matumizi ya ya game, mbali na hayo laptop hii inakuja na sifa nzuri sana kwa mtu yoyote ambaye anafanya kazi za graphics..

Sifa za Laptop ya Razer Blade 15

 • CPU: Hexa-core 2.2GHz Intel Core i7-8750H
 • Graphics: Nvidia GeForce GTX 1070
 • RAM: 16GB of 2,667MHz DDR4
 • Screen: 15.6-inch, FHD (1,920 x 1,080) LED backlit anti-glare
 • Storage: 512GB SSD

8. Acer Predator Helios 300

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kucheza game hasa kwenye laptop basi kwa sasa ni vyema kutafuta laptop mpya ya Acer Predator Helios 300. Laptop hii ni beast hasa ikija katika swala zima la games, Laptop hii pia inakuja na sifa nyingine kubwa ya kudumu na chaji kwa muda mrefu. Mbali na hayo kama unataka laptop ya kisasa yenye kufanya karibia kila kitu basi hii ni yako.

Sifa za Laptop ya Acer Predator Helios 300

 • CPU: Intel Core i7-8750H (hexa core 2.2GHz)
 • Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 + Intel UHD Graphics 630
 • RAM: 16GB DDR4
 • Screen: 15.6-inch, Full HD
 • Storage: 256GB SSD

7. Dell XPS 15 2-in-1

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Dell XPS 15 2-in-1 ni moja kati ya laptop bomba sana sana kuwa nayo. Mbali ya kuwa ni laptop yenye uwezo wa 2 in 1 lakini laptop hii pia ina nguvu sana hasa kwenye upande wa Graphics. Mbali ya yote Dell XPS 15 2-in-1 ni moja kati ya luxury laptop ambazo zinapatikana kwa bei nafuu zaidi.

 • CPU: Intel Core i5-i7
 • Graphics: Radeon RX Vega M GL Graphics with 4GB HMB2 Graphics Memory
 • RAM: 8GB
 • Storage: 512GB PCIe SSD

6. Microsoft Surface Laptop 2

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Microsoft Surface Laptop 2 ni laptop nyingine kutoka kampuni ya Microsoft, laptop hii inakuja na uwezo mzuri kiasi. Sababu ya laptop hii kuingia kwenye list hii ni bei yake, Laptop hii inauwezo mzuri pia pamoja na muundo wake ni wa kisasa kabisa.

Sifa za Laptop ya Microsoft Surface Laptop 2

 • CPU: Intel Core i5 – i7
 • Graphics: Intel UHD Graphics 620
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 13.5-inch PixelSense (2,256 x 1,504)
 • Storage: 128GB, 256GB, 512GB or 1TB SSD

5. MSI GS65 Stealth

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kila mara unapo waza kucheza game kwenye laptop basi ni vyema kuwaza laptop hii ya MSI GS65 Stealth. Inawezekana kabisa hujawahi kusikua kuhusu laptop hii lakini kwa mujibu wa tovuti mbalimbali laptop hii ni moja kati ya laptop zenye uwezo mzuri sana kwa kucheza game ya aina yoyote.

Sifa za Laptop ya MSI GS65 Stealth

 • CPU: Intel Core i7
 • Graphics: Nvidia GeForce GTX 1070 (8GB GDDR5X VRAM, Max-Q)
 • RAM: 16GB
 • Screen: 15.6-inch FHD (1,920 x 1,080) anti-glare, wide-view 144Hz panel
 • Storage: 512GB M.2 SSD
Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020)

4. Asus ZenBook Flip S UX370

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda kutumia laptop nyembamba na nyepesi basi laptop hii ya Asus ZenBook Flip S UX370 ni laptop nzuri sana kwako. Laptop hii inakuja na uwezo mkubwa sana na pia ni moja kati ya laptop pekee kwenye list hii inayotumia processor za Kaby Lake R 8th-generation processor, ukweli laptop hii ni bora sana kuwa nayo kwa mwaka 2018 n- 2019.

Sifa za Laptop ya Asus ZenBook Flip S UX370

 • CPU: Intel Core i7-8550U
 • Graphics: Intel UHD Graphics 620
 • RAM: 16GB
 • Screen: 13.3-inch full HD touchscreen
 • Storage: 512GB PCIe SSD

3. Huawei MateBook X Pro

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Hivi karibuni kampuni ya Huawei ilizindua laptop yake mpya ambayo ni Huawei MateBook X Pro, laptop hii ni toleo la pili la laptop kutoka Huawei na ni kweli kuwa laptop hii ni bora sana. Laptop hii inakuja na muundo mzuri sana pamoja na kioo kikubwa bila kusahau uwezo wake wa kudumu na chaji pamoja na kamera yake ya kisasa iliyojificha kwenye keyboard ya laptop hii. Kama unatfuta laptop yenye uwezo mzuri basi Huawei MateBook X Pro ni laptop nzuri sana kufunga nayo mwaka 2018.

Sifa za Laptop ya Huawei MateBook X Pro

 • CPU: 8th generation Intel Core i5 – i7
 • Graphics: Intel UHD Graphics 620 , Nvidia GeForce MX150 2GB GDDR5
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 13.9-inch 3K (3,000 x 2,080)
 • Storage: 512GB SSD

2. Apple MacBook Pro Touch Bar 13-inch 2018

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatafuta laptop yenye uwezo wa kufanya karibia kila kitu basi MacBook Pro ya mwaka 2018 ni laptop bora sana kwako. Laptop hii mbali ya kuwa bora zaidi, pia imeboreshwa sana tofauti na toleo la Macbook ya mwaka 2017, Kama wewe ni mmoja wa wabunifu wa programu na michoro mbalimbali hakika Apple MacBook Pro with Touch Bar 13-inch 2018 ni laptop bora sana kwako kwa mwaka huu 2018 – 2019.

Sifa za Laptop ya Apple MacBook Pro with Touch Bar 13-inch 2018

 • CPU: Quad-core Intel Core i5 – i7
 • Graphics: Intel Iris Plus Graphics 655
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 13.3-inch, (2,560 x 1,600) IPS
 • Storage: 128GB – 2TB PCIe 3.0 SSD

1. Dell XPS 13 (2018)

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Laptop Bora Kwa Mwaka 2018

Kama wewe umekuwa msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech na kama wewe ni mmoja wa watu wanaojua laptop basi lazima utakubaliana na mimi kwamba Dell XPS 13 2018 ni moja kati ya laptop bora sana hadi sasa. Laptop hii inakuja na uwezo mkubwa sana na pia ni moja kati ya laptop kwenye chache kwenye list hii zenye kioo chenye uwezo wa 4K, kifupi ni kuwa Dell XPS 13 ndio laptop bora kwa mwaka 2018.

Sifa za Laptop ya Dell XPS 13

 • CPU: 8th generation Intel Core i5 – i7
 • Graphics: Intel UHD Graphics 620
 • RAM: 8GB – 16GB
 • Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) – 4k (3840 x 2160)
 • Storage: 256GB – 1TB SSD

Na hizo ndio laptop bora za mwaka 2018, najua wengi wenu mtauliza bei za laptop hizi na hivyo ni vyema nikwambie habari njema kuwa, kwa sasa tunafanya ushirikiano na maduka makubwa ya laptop afrika mashariki kwaajili ya kukupa bei ambazo zitakuwa ndio halisi kabisa kwa asilimia 100. Pia utaweza kujua ni wapi utapata laptop hizi ili uweze kwande kununua laptop hiyo moja kwa moja, kitu cha msingi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tutakuhabarisha pindi tutakapo weka bei pamoja na sehemu ya kununua laptop hizi.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments