Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook Air

Hili ndilo toleo jipya la laptop mpya za MacBook Air
Laptop Mpya ya MacBook Air Laptop Mpya ya MacBook Air

Wakati tukiwa bize na uzinduzi wa kampuni ya kwanza ya kutengeneza simu Tanzania, huko nchini marekani hivi leo kampuni ya Apple imezindua bidhaa zake mpya. Bidhaa hizo ni pamoja na laptop mpya za MacBook Air pamoja na tablet mpya za iPad.

  • Sifa za MacBook Air 2018

Tukianza na kwa upande wa MacBook Air, laptop hiyo inakuja na kioo cha inch 13.3 ambacho pia kinakuja na Resolution ya 2560 x 1600 pamoja na teknolojia ya Retina Display, vilevile laptop hiyo mpya inakuja na kingo nyembamba zaidi ya laptop ya toleo lililopita. Mbali na hayo laptop hii inakuja na muundo mzuri sana huku ikisemekana kuonyesha rangi zaidi kwa asilimia 48 zaidi kuliko toleo la awali, huku ikisemekana kuwa laptop hii ni nyembamba na nyepesi zaidi.

Advertisement

  • Processor, RAM na Ukubwa wa Hard Disk au SSD

Tukiangalia sifa za laptop hii, MacBook Air 2018 inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya 8th-gen Intel dual-core i5 processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 16 pamoja na ukubwa wa ndani wa Terabyte (TB) 1.5. Mbali na hayo kwa mujibu wa Apple laptop hiyo sasa inadumu na chaji masaa 12 ukiwa unaitumia kufungua kurasa mbalimbali mtandaoni, pamoja na masaa 13 kama unatumia kuangalia Movie kupitia iTunes.

  • Keyboard na TrackPad

Vilevile laptop hii inakuja na keyboard mpya ambayo ni 4th generation butterfly type ambayo inatengenezwa kisasa kabisa huku kila kitufe kikiwa na uwezo wa kuwaka taa pekee yake tofauti na laptop za mwanzo ambazo zinatumia taa moja kwenye keyboard nzima. Vilevile Apple imeleta sehemu ya Touch ID kwenye laptop hiyo ambayo unaweza kuitumia kufanya manunuzi mtandaoni au kufungua tovuti mbalimbali pamoja na laptop yenyewe. Pia MacBook Air hii mpya inakuja na TrackPad (Mouse iliyoko kwenye laptop hiyo) ambayo sasa imetengenezwa kwa teknolojia mpya ambayo itafanya ibonyezeke kwa urahisi na kwa haraka.

  • Spika

Pamoja na hayo yote kampuni ya Apple imefanya maboresho kwenye upande wa spika za laptop hii ambazo sasa zinakuja na uwezo mkubwa, kwa  mujibu wa Apple  spika za laptop hii mpya zitakuwa na uwezo wa kutoa sauti ya Bass mara mbili zaidi ya matoleo ya laptop za MacBook Air yaliyopita.

Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook Air
MacBook Air 2018

TSh 3,404,000

Pins
  • Viunganishi na Muundo

Kwa upande wa viunganishi laptop Hii inakuja na sehemu tatu za Thunderbolt, hizi ni tofauti kidogo na sehemu zile za kawaida za USB, na kupitia sehemu hizo unaweza kutumia kuchomeka kioo chenye uwezo wa 5K, au hata kadi ya kuongeza uwezo wa graphics. Mbali na viunganishi hivyop Kava la laptop hii mpya limetengenezwa kwa aina mpya ya material ya Aluminum ambayo yanafanya laptop hii kuwa nyepesi zaidi kwa asilimia 17 huku ikiwa na uzito wa kilo 1.24.

  • Bei ya MacBook Air 2018

Kwa upande wa bei laptop hii inategemewa kuanza kuuzwa kuanzia tarehe 7 mwezi ujao (November) huku kampuni ya Apple ikidai kuwa laptop hii ya MacBook Air ya mwaka huu ndio laptop ya bei rahisi zaidi, huku bei yake ikianzia dollar za marekani $1,199 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 2,745,000 bila kodi, kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kupanda au kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha vya tarehe husika.

Na hiyo ndio laptop mpya ya MacBook Air 2018 ambayo imezinduliwa leo tarehe 30 mwezi Oktoba 2018 huko nchini marekani, ambapo pia Apple ilifanyika uzinduzi wa tablet zake mpya za iPad Pro 11 pamoja na iPad Pro 12.9 ambazo tumeziangalia kwa undani kwenye makala inayofuata.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use