in

Kampuni ya Microsoft Kutangaza Laptop Mpya ya Surface Leo May 2

Kaa tayari kwa laptop mpya kutoka kampuni ya Microsoft leo tarehe 2 mwezi may

Microsoft-Surface-Laptop
PICHA WAIKINGCAT / TWITTER

Kampuni maarufu ya Microsoft leo inategemea kufanya mkutano wake mkubwa huko nchini marekani huku wapenzi wa bidhaa kutoka kwenye kampuni hiyo wakingoja kutangazwa kwa bidhaa mpya za mwaka 2017 kutoka kwenye kampuni hiyo inayojulikana sana kwa utengenezaji wa programu za Windows.

Hata hivyo katika mkutano huo ambao utafanyika leo huko New York City unategemewa kusindikizwa na uzinduzi wa toleo jipya la programu ya Windows 10 pamoja na lengo la mkutano huo yani uzinduzi wa laptop mpya ya Surface. Laptop hii ambayo imevuja picha zake kwenye mtandao wa Twitter leo kabla haijatangaza inasemekana kuja na kioo cha inch 13.5 chenye teknolojia ya PixelSense display pamoja na keyboard ya alcantara keyboard ambayo pia inatumika kwenye laptop ya premium Surface Pro, laptop hiyo mpya pia inasemekana itatoka kwa rangi nne za platinum, burgundy, cobalt blue, pamoja na graphite gold.

Kuhusu processor pamoja na sifa zingine bado haijajulikana itakubidi kusubiri uzinduzi wa laptop hiyo ambao utafanyika leo mida ya 4:30 PM kwa saa za Afrika Mashariki. Kukuleta uzinduzi huo tutakuwa live tukionyesha mkutano huo hapa hapa kupita tovuti yetu ya Tanzania Tech hivyo usikae mbali ili kujua yote yatakayo jiri kwenye mkutano huo.

Hii Ndio Sababu ya Laptop Nyingi Kuharibika Haraka

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.