Mwanzilishi Mwenza wa Vine na HQ Trivia Afariki Duniani

Inasemekana chanzo cha kifo chake ni utumiaji wa madawa ya kulevya
Colin Kroll Colin Kroll
Colin Kroll

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ aliyekuwa mwanzilishi mwenza wa mtandao wa kijamii wa Vine pamoja na game ya HQ Trivia Colin Kroll, amekutwa akiwa amefariki kwenye apartment yake huko New York nchini Marekani. Kwa mujibu wa TMZ, pembeni ya mwili wa mwanzilishi huyo kumekutwa dawa za kulevya aina ya Paraphernalia hivyo inasemekna kuwa chanzo cha kifo cha mwanzilishi huyo huenda ikawa ni Overdose.

Kwa wale ambao ni wahenga kidogo najua mtakuwa mnajua kuhusu mtandao wa Vine ambao uligunduliwa mwaka 2012 na Dom Hofmann, Rus Yusupov na Colin Kroll huku mtandao huo kipindi hicho ukiwa ni mtandao maalum kwa ajili ya kushare Video fupi.

Logo ya mtandao wa Vine
Logo ya mtandao wa Vine

Mara baada ya ugunduzi Mwaka huohuo 2012 mtandao wa kijamii wa Twitter ulinunua mtandao wa Vine kwa dollar za marekani milioni 30 na kufanya mtandao huo kuwa sehemu ya mtandao wa Twitter. Mwaka uliofuatia mgunduzi kiongozi wa mtandao huo wa Vine, Dom Hofmann alitangaza kuachana na kampuni ya Twitter na kumuacha Colin Kroll akiwa kiongozi wa mtandao huo.

Advertisement

Baadae Kroll alifukuzwa kazi na Twitter na ilipofika mwaka 2016 Twitter ilitangaza rasmi kuzima mtandao wa Vine kutokana na kutofanya vizuri kwa mtandao huo ambao kipindi hicho ulikuwa ukishindana na mtandao kama YouTube na Instagram.

Mwaka 2017 Rus Yusupov na Colin Kroll waliungana tena na kuleta game mpya ya HQ Trivia game ambayo inahusika kujibu maswali yanayoulizwa mubashara na kuweza kujishindia pesa hadi dollar za marekani $150,000. Kwa bahati mbaya HQ Trivia haifanyi kazi kwa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla hivyo don’t think about it.

Rus Yusupov (kushoto) na Colin Kroll (kulia)
Rus Yusupov (kushoto) na Colin Kroll (kulia)

Anyway Hata hivyo Game hiyo ya HQ Trivia ilianza kukubwa na misukosuko mara baada ya kukosekana kwa wawekezaji kutoka na kuripotiwa kwa tabia mbaya aliyokuwa nayo Colin Kroll juu ya wafanyakazi wa kike ndani ya kampuni hiyo. November mwaka huu inaripotiwa kuwa tabia ya mwanzilishi huyo ilizidi kuwa mbaya zaidi siku chache kabla ya kupewa cheo cha Mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo.

Game hiyo kipindi cha karibuni imeripotiwa kupungua kwa watumiaji kutokana na kile kilicho elezwa kuwa ni kuendelea kwa tabia mbaya ya Colin Kroll kitu mbacho awali ndio kilifanya afukuzwe kazi na Twitter. Kroll amefariki akiwa na umri wa miaka 34 na inasemekana ailishawahi kufanya kazi kwenye makampuni kama Yahoo na Jetsetter zote za nchini marekani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use