Kitendo Gani Umaliza Data Kati ya Kustream au Kudownload

Je wakati gani bando hutumika zaidi kati ya kudownload au kustream..?
Kustream au kudownload Kustream au kudownload

Linapokuja swala la kutumia data ni wazi kila mtu huwa makini sana, hili linakuja kutokana na mitandao ya simu kubadilisha vifurushi vya internet kila mara na hii upelekea huduma za internet kuwa ghali zaidi kadri siku zinavyokwenda.

Sasa kuliona hili leo Tanzania Tech tunakupa ufafanuzi ambao pengine unaweza kukusaidia kuweza kutunza data kwenye kifaa chako ili kudhibiti matumizi makubwa ya internet unayofanya kila siku. Ufafanuzi huu unahusu vitendo viwili ambavyo wengi wetu hufanya kila siku tunapo nunua bando au data. Vitendo hivyo ni ku-stream na ku-download.

Kumekuwa na maswali mengi sana kuhusu vitendo hivyo lakini leo tutajibu maswali machache ambayo mara nyingi yamekuwa yakiwachanganya watu watu wengi. Lakini kumbuka swali kubwa kwenye maka hii linauliza, ni kitendo gani kinacho maliza zaidi bando kati ya kustream au kudownload..?

Advertisement

Kuna Tofauti Gani Kati ya Kustream na Kudownload

Kwa kuanza labda nikwambie kustream na kudownload ni vitendo ambavyo vinafanana kwa namna moja ama nyingine kwani wakati vitendo hivi vinatokea hatua ya kupokea file kutoka kwenye internet kuja kwenye simu yako hufanyika mara zote. Tofauti kubwa iliyoko kwenye vitendo hivi ni kuwa, kustream una angalia au kusikiliza muziki pale file linapo patikana kupitia internet, na kudownload unaangalia video au muziki pale file linapomaliza kuhifadhiwa kwenye kifaa chako.

Pia tofauti nyingine ni kuwa pale unapo maliza kitendo cha kudownload unabaki na copy ya file husika, wakati pale unapo maliza kitendo cha kustream file zilizo hifadhiwa kwenye kifaa chako hufutika mara moja hivyo pale unapotaka kuangalia au kusikiliza file hilo kwa mara ya pili inabidi kutumia data kwa mara ya pili.

Je Kiasi cha Data (Bando) Kinachotumika Kustream na Kudownload ni Sawa..?

Kitu kingine ambacho ni muhimu wewe kujua ni kuwa kustream na kudownload hutumia kiasi sawa cha data lakini endapo file linakuja na format tofauti basi hatua ya kustream au kudownload huweza kuchukua bando nyingi zaidi. Ili uweze kuelewa labda tuangalie mfano huu, Kwa mfano unaangalia video kupitia mtandao wa YouTube, video hiyo inakuja kwa format tofauti kati ya 720p na 1080p, mara nyingi mtandao wa YouTube hutumia format ambayo ni sahihi kwa simu yako au kifaa chako kama simu yako inasupport 1080p basi video huweza kujiseti na kwenda kwenye mfumo huo ambao hutumia data (bando) nyingi zaidi kuliko 720p.

Kwenye kudownload ni hivyo hivyo kwani mtu anapo pakua video yenye format ya 1080p basi kuweza kutumia kiasi sawa cha data na yule aliyetumia bando kustream video ya 1080p, hivyo utaona tofauti inakuja kwenye aina ya file unalo download au unalo stream.

Je ni Kitendo Gani Umaliza Data Kati ya Kustream na Kudownload..?

Sasa baada ya hapo labda ni kupe hitimisho kwa kujibu swali hili, Kustream na Kudownload kwenye upande wa matumizi ya Bando huwa sawa endapo file linalokuwa stream au linalodownloadiwa ni sawa. Pia kiasi cha bando huwa sawa zaidi pale ambapo file hilo linapokuwa halina quality tofauti.

Japokuwa najua inawezekana ufafanuzi huu usikutoshe lakini nachokushauri ni kuwa maranyingi angalia matumizi ya file kabla ya kuamua kuchagua moja kati ya vitendo hivyo. Kama unajua unataka kurudia kuangalia au kusikiliza file hilo basi hakikisha unadownload file hilo na kama unataka kuangalia maramoja basi unaweza kuchagua kitendo cha kustream.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use