in

Huawei Mbioni Kuzindua Simu Mpya ya Huawei Mate 20

Zifahamu hizi hapa sifa za awali za Simu mpya ya Huawei Mate 20

Simu mpya ya Huawei Mate 20

Kampuni ya Huawei iko mbioni kuja na simu yake mpya ya Huawei Mate 20, Kama ilivyokuwa kwenye simu za Huawei P20 na P20 Pro, simu hiyo mpya ya Huawei Mate 20 nayopia inatarajiwa kuangalia zaidi kwenye upande wa kamera pamoja na mfumo wa AI.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena simu hiyo mpya ya huawei Mate 20 inatarajiwa kuja na kamera tatu kwa nyuma huku zikiwa kwenye mtindo mpya tofauti na ambavyo watu wamezoea au jinsi simu nyingi zinavyokuwa.

Mbali na hayo simu hii mpya ya Huawei Mate 20 inatarajiwa kuja na mfumo wa Android 9 Pie, Processor kutoka kwa Huawei ya HiSilicon Kirin 980 inayo saidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128. Kioo cha Huawei Mate 20 kinakuja na ukubwa wa inch 6.3 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED, ambacho pia kinakuja na resolution ya 2244×1080.

Simu hii inatarajiwa kuja kwa matoleo matatu ikiwa pamoja na Huawei Mate 20, Mate 20 Pro na Huawei Mate 20 Porsche Edition ambazo zote zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao tarehe 16 october 2018.

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Kwa sasa ili kujua zaidi kuhusu simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea uzinduzi wa simu hii mubashara kabisa kupitia hapa hapa.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments