Kampuni ya HTC Yazindua Simu Mpya ya HTC U12 Plus

Simu hii mpya inakuja na uwezo wa kamera nne kwa ujumla
Simu mpya ya HTC U12 Plus Simu mpya ya HTC U12 Plus

Kampuni ya HTC imerudi tena rasmi na simu mpya ambayo ni toleo jipya la simu za mwaka jana za HTC 12 na HTC 12 Plus. Kampuni hiyo yenye makao yake makuu huko nchini Taiwan leo imetambulisha simu hiyo mpya ya HTC U12 Plus ambayo inakuja na maboresho mapya tofauti na simu za mwaka jana za HTC 12.

Moja ya maboresho ambayo ni rahisi sana kuona kwenye simu hiyo mpya ya HTC U12 Plus ni pamoja na jumla ya kamera nne, yaani kamera mbili kwa nyuma pamoja na kamera mbili kwa mbele. Simu hii pia inakuja na teknolojia ya Edge Sense 2, aina mpya ya teknolojia ambayo ilitambulishwa kwenye simu za HTC 12, teknolojia hii itakuwezesha kutumia simu hiyo kwakubonyeza kingo za kushoto au kuliza za simu hiyo.

Mbali na hayo, simu hiyo mpya pia inakuja na kioo kikubwa zaidi ya simu za HTC 12 za mwaka jana, HTC U12 Plus inakuja na kioo cha inch 6.0 chenye uwezo wa HDR10 pamoja na teknolojia ya Super LCD6 capacitive touchscreen. Kioo cha simu hii pia kina uwezo wa kuonyesha resolution ya 1440 x 2880 pixels, pamoja na Aspect ratio ya 18:9 ratio (~537 ppi density).

Advertisement

Mbali na hayo kingine cha muhimu kufahamu kuhusu simu hii ni kuwa, simu hii inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi (IP68 waterproof) ambayo inasaidia simu hii kuto kuingia maji kwa muda mfupi. Sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.

Sifa za HTC U12 Plus

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya Super LCD6 display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 2880 pixels, 18:9 ratio (~537 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo) itakuwa na uwezo wa Android P
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Kwa rangi ya Gold na 4×1.7 GHz Kryo 385 Kwa rangi ya Silver), Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 na nyingine inakuja ikiwa na ukubwa wa GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko mbili zote zikiwa na uwezo wa Megapixel 8 zenye (f/2.0, 1.12µm), 1080p, HDR, panorama.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye uwezo wa (f/1.8, 1.4µm, Dual Pixel PDAF) na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye (f/2.6, 1.0µm), kamera zote za nyuma zinakuja na uwezo wa phase detection, laser autofocus, OIS, gyro-EIS, 2x optical zoom, pamoja na dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery yenye teknolojia ya (Quick Charge 3.0).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Translucent Blue, Ceramic Black na Flame Red.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya HTC U12 Plus

Kwa upande wa bei ya simu hii, HTC U12 Plus yenye ukubwa wa GB 64 itaanza kuuzwa kwa dollar za marekani $799 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,824,000. Kwa simu ya HTC U12 Plus yenye GB 128 itakuja ikiwa inapatikana kwa dollar za marekani $849 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,938,000. Kumbuka bei ya simu hizi inaweza kubadilika kwa Tanzania kwa sababu ya kodi na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use