in

WhatsApp Kuja na Sehemu Mpya ya High Priority Notifications

Sasa utaweza kuweka juu taarifa zote za meseji za WhatsApp

WhatsApp Kuja na Sehemu Mpya ya High Priority Notifications

Hivi karibuni kupitia programu ya WhatsApp Beta, WhatsApp ilionekana kufanya majaribio ya sehemu mpya ambapo unaweza kurudisha picha zilizo futika kwenye programu ya WhatsApp. Lakini kama haitoshi hivi karibuni tena, inasemekana kuwa WhatsApp inafanya majaribio ya sehemu mpya ya High Priority Notifications.

Kwa mujibu wa tovuti ya WABetaInfo sehemu hiyo ipo kwenye programu ya Majaribio ya WhatsApp ambapo sehemu hiyo itakusaidia kuweza kuweka kutanguliza juu ujumbe wa taarifa zote za programu ya WhatsApp. Yaani kinacho tokea ni kuwa unapo washa sehemu hii, utaweza kupata ujumbe wa WhatsApp ukiwa juu wa kwanza kwenye sehemu yako ya kupata ujumbe iliyoko juu ya simu yako na utaweza kuona jumbe hizo za WhatsApp kabla ya ujumbe wa programu nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa hizo sehemu hiyo inauwezo wa kufanya kazi kwenye simu za Android zenye toleo la Android 5.0 (Android Lollipop) na kuendelea, ili kuwasha sehemu hiyo utaingia kwenye Settings za programu ya WhatsApp kisha bofya Notification kisha chagua Use High priority notifications.

Kama wewe unayo programu ya majaribio ya WhatsApp Beta kwa mfumo wa Android unaweza kuwasha sehemu hiyo hivi sasa, hakikisha una update programu hiyo kabla ya kufanya hivyo.

March : Jaribu Apps Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Kwa watumiaji wa Kawaida wa WhatsApp itakubidi kusubiri kidogo ili kuweza kupata sehemu hii kwenye simu yako ya Android. Vilevile inasemekana pia ile sehemu ya ma-admin kuweza kuwaondoa ma-admin wengine bila taarifa inatarajiwa kuja siku za karibuni.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment