Tecno F1, F2 na F3 Simu za Kwanza za Tecno Zenye Android Go

Simu hizi mpya za F1, F2 na F3 zinategemewa kuuza kwa bei nafuu zaidi
Tecno F1, POP 1, F2 na Tecno F3 Tecno F1, POP 1, F2 na Tecno F3

Wakati tamasha la uzinduzi wa simu za Tecno Camon X unaendelea, Habari tulizo zipata ni kuwa Tecno inakuja na simu mpya za Tecno F1, F2 na Tecno F3 simu hizi zitakuwa za kwanza kabisa kutoka kampuni ya Tecno kutumia mfumo wa uendeshaji wa Android Go.

Simu hizi za Tecno F1, F2 na F3  ambazo pia zinajulikana kama (POP 1) zitakuja kwa mtindo mpya wa kioo kizima au Full Display yaani simu hizi zitakuwa na Aspect Ratio ya 18:9, ambapo zitakuwa na muonekano wa kisasa na ukingo mdogo. Kwa mujibu wa Tecno simu hizi zitakuja na uwezo mkubwa wa processor pamoja na kamera nzuri sana.

Tukiwa kwenye upande huo huo wa Kamera, Tecno F1 na Tecno F2 zinakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 2 wakati Tecno F3 inakuja na kamera ya Megapixel 5, Simu zote hizi kwa nyuma zinakuja na kamera yenye uwezo wa Megapixel 5 pamoja na flash ya Dual Flash.

Advertisement

Kama nilivyo eleza awali simu hizi zitakuja na mfumo mpya wa uendeshaji wa Android Go na inategemewa kuwa zitakuja zikiwa zinatumia mfumo mpya wa Oreo yaani Android Go Oreo. Kwa upande wa ukubwa wa ndani bado haijajulikana rasmi lakini inawezekana simu hizi kuja na ukubwa wa kuanzia GB 8 hadi GB 16. Kwa upande wa RAM inategemewa simu hizi zitakuja na RAM ya GB 1 au GB 2 kwani hiyo ndio maana halisi ya mfumo wa Android Go.

Zifahamua Hapa Sifa za Simu Hizi za Tecno F1, Tecno F2 na Tecno F3

Kwa upande wa bei tegemea simu hizi zitakuja sokoni zikiwa na Bei nafuu zaidi kwani mara nyingi simu zinazotumia mfumo huu wa uendeshaji huwa ni simu za bei nafuu ukilinganisha na simu zenye kutumia mfumo wa kawaida.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use