Soko la Programu za iOS (App Store) Lafikisha Miaka 10

Historia fupi ya soko la programu za iOS App Store
App store miaka 10 App store miaka 10

Tarehe kama ya leo miaka 10 iliyopita soko la programu za iOS App Store lilizinduliwa rasmi, kipindi hicho soko hilo lilikuwa na programu 500 kwaajili ya simu za iPhone huku kukiwa na wabunifu wachache sana wa programu hizo.

Fast forward hadi sasa (2018), soko la App Store lina programu zaidi ya milioni 2 huku kukiwa na wabunifu waliosajiliwa na Apple zaidi ya milioni 20 huku soko hilo likikadiriwa kuingiza faida zaidi ya bilioni $100 za marekani. Lakini pamoja na hayo mafanikio hayo hayakuanza ghafla kwani hata ukiangalia kipindi hicho app zilizokuwa zinashika chati ya app bora za mwaka utaona kweli soko hilo limeanzia mbali.

Hapo juu ni takwimu za app zilizoshika nafasi ya App kumi bora za mwaka kati ya mwaka 2007 hadi mwaka 2008. Kama unavyoona app bora ya kununuliwa wakati huo mwaka 2008 ilikuwa ni App ya Kio Pond, kama wewe ni muhenga basi lazima utakuwa unaijua app hiyo kwani ndio ilikuwa kitu kizuri cha kungaza kwenye mfumo wa iOS wakati huo.

Advertisement

Kama wewe ni kizazi kipya na unataka kujua Koi Pond ni App gani basi unaweza kuangalia video hapo chini. Kwa wale wahenga nadhani hapa lazima utakuwa umekumbuka mbali kwa namna moja ama nyingine.

Tukiachana na hayo ni wazi soko la App store limetoka mbali sana na wakati huo sidhani kama kuna mtu alidhani soko hili lingekuja kutegemewa na watumiaji zaidi ya Milioni 10 wenye vifaa vya iPhone, iPad na iPod. Picha hapo chini ni picha ya soko hilo la App Store miaka 10 iliyopita.

Hadi sasa mwaka huu 2018 programu ambazo ndio programu bora kwenye soko hilo ni programu zifuatazo.

Application bora kwenye soko la App Store Hadi Sasa (2018)

 1. Facebook
 2. Facebook Messenger
 3. YouTube
 4. Instagram
 5. Whatsapp Messenger
 6. Google Maps
 7. Snapchat
 8. Skype
 9. WeChat
 10. QQ

Game bora kwenye soko la App Store Hadi Sasa (2018)

 1. Candy Crush Saga
 2. Subway Surfers
 3. Fruit Ninja
 4. Clash of Clans
 5. Honour of Kings
 6. Minion Rush
 7. Angry Birds
 8. Temple Run 2
 9. Temple Run
 10. Asphalt 8: Airborne
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use