Sasa Angalia Video za Youtube Bila Internet kwa Kutumia Youtube Go

Google kutoa Programu mpya ya Youtube go programu hiyo itakuwezesha kuangalia video bila internet
youtube-Go App youtube-Go App

Kama unataka kuhifadhi video zako za youtube ili kuangalia baadae lakini unapata shida sasa yote hayo yataisha kwani hivi karibuni kampuni ya Google inategemea kutambulisha programu yake mpya ambayo inategemewa kuitwa Youtube Go.

Youtube Go ni programu ambayo itakusaidia kuhifadhi video zako za Youtube kwa mpangilio wa kisasa na kwa kutumia memory ya simu yako ili kukuwezesha kuangalia video zako baadae bila kutumia internet (bando). Tofauti na sehemu iliyo kwenye programu ya Youtube ya sasa, programu hiyo mpya ya Youtube Go itakuwezesha kushiri na wengine video hizo kwa njia ya bluetooth moja kwa moja kutoka kwenye programu hiyo.

Katika utambulishi wa programu hiyo uliofanyika huko New Delhi India, kampuni ya Google ilidhibitisha kuwa programu hiyo mpya itaanza kupatikana kwenye nchi hiyo alafu baadae ndipo itakapokuja kwenye nchi zingine. Kwa sasa kampuni ya Google inchini india inafanya usajili wa awali kwa wale wanaopenda kujaribu programu hiyo pale tu itakapotoka.

Advertisement

Kama unataka kujua pale programu hii itakapo fika Tanzania endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use