Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Habari Kuhusu Aliye Wapiga Risasi Wafanyakazi wa YouTube

Ripoti kamili kuhusu mtu aliye vamia kwenye jengo la Makao makuu ya YouTube
Youtube shooting Youtube shooting

Kama ulikuwa mmoja ya wafuatiliaji wa Tanzania Tech jana usiku ni wazi ulipata taarifa kuhusu kuvamiwa kwa jengo la makao makuu ya mtandao wa YouTube na kupigwa risasi kwa wafanyakazi wa nne wa YouTube wakiwa ndani ya jengo hilo ambalo liko huko San Bruno nchini marekani. Sasa baada ya kutafuta habari zaidi ya tukio zima hii ndio habari kamili kuhusu tukio hilo.

Advertisement

Kama tulivyokujuza kwenye ripoti zilizo pita mtuhumiwa ni mwanamke na inaripotiwa kuwa anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 39 na 40 na anatambuliwa kwa majina matatu ya Nasim Najaf Aghdam na ni mwanamke mwenye asili ya Kiajemi au Persian.

Kuhusu Tukio zima, Hapo jana (usiku kwa saa za afrika mashariki) na mchana kwa saa za marekani, Nasim aliingia na silaha (bunduki aina ya pistol) kwenye jengo la makao makuu ya mtandao wa YouTube na kuanza kufyatua risasi kwa wafanyakazi wa Mtandao huo walio kuwepo ndani ya jengo hilo.

Aidha ripoti baada ya tukio kutoka kwenye mitandao mbalimbali kama BBC, zilibainisha baada ya mshtakiwa huyo kufanya tukio hilo alijipiga risasi na kupoteza maisha ndani ya Jengo hilo. Hata hivyo ripoti zilibainisha kuwa watu wanne walijeruhiwa na hakuna mtu aliye poteza maisha zaidi ya muhusika wa tukio hilo ambaye ndio anae tambuliwa kama Nasim Najaf Aghdam.

Je Nasim Najaf Aghdam ni nani .?

Habari zaidi zinasema Nasim, alikuwa ni mmoja wa watu wengi wanao tegemea mtandao wa YouTube kuendeleza harakati zao za kila siku na kwa upande wa Nasim inasemekana kuwa yeye alikuwa ni Blogger pamoja na mwana harakati wa kutetea haki za wanyama, pamoja na mwana mazoezi na hiyo ni kwa mujibu wa touvti yake.

Hata hivyo kabla ya kurasa zake za mitandao ya kijamii ya YouTube na Instagram hazijafungwa Nasim alikuwa anajulikana kama ‘Nasim the Persian Azeri female vegan bodybuilder, pia  animal rights activist promoting healthy and humane living.”

Kwa mujibu wa ripoti inasemekana kuwa Nasim alikuwa anapakia video kwenye mtandao wa YouTube zenye maudhui ambayo yalionyesha maoni yake juu ya mada kama dhana ya uhuru wa kujieleza, kupinga ubaguzi katika nchi za magharibi pamoja na haki za wanyama na video nyingine nyingi. Inasemekana pia alikuwa akitumia ukurasa wake wa Instagram kuweka picha za kutisha za wanyama waki nyanyaswa ili kuongeza ufahamu kwa watu kuhusu haki za wanyama.

Inasemekana kuwa hivi karibuni Nasim alikua akihisi kuwa mtandao wa Youtube hamtendei haki kwa kusema kuwa YouTube ilikuwa ikibagua video zake na kuzifungia kutokana na kutokuwa na mauthui yasiyo sahihi, kitendo ambacho yeye alikipinga na kusema ni unyanyasaji.

https://twitter.com/DivineNeet/status/981360176996540417

Sasa inasemekana kuwa moja ya chanzo kilicho mshinikiza Nasim kufanya tukio hilo hapo jana ni pamoja na channel yake ya YouTube inayojulikana kama “Nasime Wonder1” ambayo ilikuwa na wafuatiliaji zaidi ya 5000 huku video zake kwa ujumla zikiwa na view zaidi milioni moja. Hata hivyo inasemekana kuwa kutokana na mabadiliko ya hivi karibu ya matangazo ya YouTube, channel yake hiyo iliondolewa matangazao na kufanya kupungua kwa view na mapato ya channel kitendo ambacho kinasemekana kilimchukiza sana Nasim.

Hata hivyo inasemekana kwenye moja ya video zake kwenye channel hiyo ambayo sasa imefungwa Nazim alisikika akisema kwa hasira, “I am being discriminated on and filtered on YouTube and I am not the only one”, akiwa na maana “Nina baguliwa na kuchujwa kwenye mtandao wa YouTube na sio mimi pekee” Vilevile inasemekana kuwa Nazim aliandika akionyesha msisitizo “There is no equal growth opportunity on YOUTUBE or any other video sharing site, your channel will grow if they want to!!!!!”.

Habari kutoka mtandao wa Mercury News zinasema kuwa, baba mzazi wa Nazim alisha wahi kutoa ripoti kwa polisi kwa kuhofia mwanae kwenda kwa nia mbaya kwenye makao makuu ya ofisi hizo za mtandao wa YouTube kutokana na mwanae kuonyesha chuki kubwa aliyokuwa nayo juu ya kampuni hiyo ya YouTube.

Kwa sasa Bado uchunguzi unaendelea tutendelea kuwaleta taarifa zaidi pindi tutakapo zipata, endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use