in

Huawei Kuja na Simu Mpya ya Huawei P20 Yenye Kamera Tatu

Simu hii pia inakuja na ukingo wa juu (Notch) kama ilivyo iPhone X

Simu ya Huawei P20
Photo by Telefoonabonnement.nl

Mwaka huu 2018, unaoneka kama ni mwaka wa kuboresha kamera kwenye simu nyingi za mkononi. Wakati tayari samsung ikiwa imezindua simu ya Galaxy S9 yenye kuboreshwa zaidi upande wa kamera kampuni ya Huawei nayo inajiandaa kuja na simu yake mpya ya Huawei P20 yenye kamera Tatu.

Kwa mujibu wa picha iliyovujishwa kwenye mtandao wa kijamii wa china Weibo, simu hiyo ya Huawei P20 inatarajiwa kuja na kamera hizo tatu kwa nyuma pamoja na ukingo wa juu (Notch) kama ilivyo simu ya iPhone X.

Simu hii ya Huawei P20 inategemewa kuja kwa ina tatu ambazo ni Huawei P20 ya kawaida, Hauwei P20 Pro pamoja na Huawei P20 Lite. Kwa sasa bado haijajulikana ni simu ipi kati ya hizi itakayokuwa na kamera tatu kwa nyumba lakini huwenda ni toleo la Huawei P20 Pro. Kwa mujibu wa tweet kutoka kwa mvujishaji Roland Quandt Huawei P20 Pro inatarajiwa kuuzwa kwa Euro €899, wakati toleo la kawaida la Huawei P20 litauzwa Euro €670, na toleo la P20 Lite litauzwa €369.

Usinunue Simu ya Android au iPhone ya Zamani

Kwa sasa tayari kumevuja picha za simu hii lakini, bado hakuna taarifa kuhusu sifa za simu hii mpya, pengine tusubirie siku ya uzinduzi wa simu hii ambayo inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 27 mwezi huu 2018.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.