Mtandao wa Instagram Kuongezewa Sehemu Mpya ya ‘Regram’

Sasa utaweza kushare post ya mtu yoyote kwenda kwenye sehemu ya Stories
Sehemu mpya ya Instagram Regram Sehemu mpya ya Instagram Regram

Hivi karibuni Instagram imekua ikifanya maboresho makubwa hasa ya sehemu ya Stories na siku chache zilizopita tumeona instagram ikileta sehemu mpya ya stories inayoitwa “Type”, lakini kama haitoshi bado instagram inazidi kuboresha sehemu hiyo na sasa inakuja na sehemu mpya ya “Regram”.

Sehemu hii itakuruhusu kuweza kushiriki picha za watu wengine na kuzituma moja kwa moja kwenye sehemu yako ya Stories. Kifupi ni kuwa sehemu hii itakuwezesha ku-repost picha mbalimbali za watu kwenda kwenye sehemu yako ya Stories ndani ya programu ya Instagram.

Advertisement

Mbali na kuruhusu watu kushare au ku-regram picha mbalimbali za watu lakini pia instagram itaruhusu kuweza kubadilisha post hizo ikiwa pamoja na kuongeza stika kuweka rangi pamoja na kupunguza (crop) picha hiyo.

Kwa sasa sehemu hii iko kwenye programu ya majaribio ya Instagram na inasemekana kuna uwezekano sehemu hii kuja kwa watumiaji wote siku za karibuni, Vilevile kwa watumiaji wa mtandao wa Instagram ambao hawatopenda kuruhusu watu ku-share post zao wanaweza kuzima sehemu hiyo kupitia sehemu ya settings ndani ya programu ya Instagram.

Bado hakuna taarifa kamili lini sehemu hii itakuja kwa watumiaji wote, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa pindi sehemu hiyo itakapo kuja kwenye smartphone yako.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use