in

Sasa Unaweza Kutumia Aina Mpya ya Instagram Stories “Type”

Sasa unaweza ku-andika maneno kwenye sehemu ya Stories kupitia sehemu ya “Type”

Aina mpya Instagram Stories Type

Hivi karibuni mtandao wa Instagram ulikua unafanyia kazi aina mpya ya stories inayoitwa Type na hatimae sasa sehemu hiyo imekamilika na unaweza kutumia kupitia programu yako ya mtandao wa Instagram.

Aina hiyo mpya ya stories ina fanana na zile za kwenye mitandao ya Facebook na WhatsApp ambapo unaweza kuandika stories kwa maneno na kushiriki na wengine kwanye akaunti yako ya mtandao wa Instagram.

Sehemu hiyo inapatikana kwa kubofya sehemu ya Stories kwenye profile yako kisha pale kamera inapo funguka angalia upande wa kulia utaona sehemu hiyo imeandikwa “Type” bofya hapo kisha andika maneno unayotaka kisha badili muandiko na rangi kwa kubofya vitufe vilivyo juu na chini kulia.

Baada ya kumaliza bofya kitufe katikati na utakuwa ume-maliza kupost aina hiyo mpya ya Stories inayoitwa “Type”. Sehemu hii tayari inapatikana kwenye programu zote za Instagram, kama bado hujaiona sehemu hiyo basi update app ya instagram kupitia soko la App Store au Play Store.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Apps (7) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2022)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments