Haya Hapa Mambo 5 Usiyo Yajua Kuhusu Kampuni ya Samsung

Haya ndio mambo ambayo pengine ulikua huyajui kuhusu Samsung
Haya Hapa Mambo 5 Usiyo Yajua Kuhusu Kampuni ya Samsung Haya Hapa Mambo 5 Usiyo Yajua Kuhusu Kampuni ya Samsung

Katika hali ya kawaida wengi wanao fuatili mambo ya teknolojia wameikuta kampuni ya Samsung, lakini ni vyema kufahamu angalau kidogo kuhusu kampuni hii ndio maana leo nimekuletea mambo haya 5 ambayo pengine ulikua hujui kuhusu kampuni ya Samsung.

  • Jina la Samsung Lina Maana ya Nyota Tatu

Nchini korea maana ya neno Samsung ni nyota tatu kwa kiswahili, mwanzilishi wa kampuni hii aliamua kuja na jina hili baada ya kuwa na ndoto ya kufanya kampuni hiyo kuwa kubwa na juu zaidi kama nyota. Ndio maana logo ya kwanza ya kampuni hiyo ina nyota tatu.

  • Logo ya Samsung Imebadilishwa Mara tatu tu

Ni kawaida sana kwa makampuni kufanya mabadiliko mbalimbali, hii inaweza ikawa mabadiliko ya kibiashara au hata mabadiliko ya muonekano lakini kwa samsung hili ni tofauti kidogo kampuni hii haijafanya mabadiliko makubwa sana ya kimuonekano kwani kampuni hii toka kuanzishwa kwake mwaka 1938 imefanya mabadiliko ya logo yake mara tatu tu tofauti na kampuni nyingia ambazo tunazijua sasa. Logo inayotumika sasa ilianza kutumika rasmi mwaka 1993.

Advertisement

  • Bidhaa ya kwanza ya Kieletroniki kutoka Samsung ni TV

Kwa sasa samsung inajulikana sana kwa utengenezaji wa vitu mbalimbali vya kieletorniki, lakini miaka ya nyuma kabla ya utengenezaji wa vifaa hivyo samsung ilikua ikifanya biashara ya usindikaji wa chakula, biashara ya nguo, bima, ulinzi na biashara nyingine za rejareja. Kufikia miaka ya 1960 kampuni hiyo ilingia kwenye biashara ya vifaa vya kielectroniki na ndipo mwaka 1970 kampuni hiyo ilifanikiwa kutoa bidhaa ya kwanza ambayo ilikua ni TV yenye rangi mbili tu nyeusi na nyeupe.

  • Jengo Refu kuliko Yote Duniani la Burj Khalifa Limejengwa na Samsung

Najua utakuwa umeshtuka kidogo lakini ni kweli, Kampuni ya samsung inajumuisha makampuni zaidi ya 80 ambayo yanafanya kazi mbalimbali ikiwemo kazi ya ujenzi. Kampuni ya Samsung C&T Ndio iliyokuwa mjenzi mkuu wa jengo hilo refu kuliko yote la Burj Khalifa ambalo lipo nchini Dubai. Hata hivyo Samsung ilishirikiana na makampuni mengine kujenga gorofa hilo.

  • Samsung Ndio Kampuni ya Kwanza Kutengeneza Simu Yenye MP3 Player

Samsung ndio kampuni ya kwanza kabisa ambayo ilifanikiwa kutengeneza simu yenye uwezo wa  MP3 na hadi kufikia mwaka 2000 samsung ilitoa simu ya Samsung SPH-M100 (UpRoar) ambayo ndio simu pekee kwa muda huo iliyokuwa na uwezo wa kusoma file za MP3.

Na hayo ndio baadhi ya mambo ambayo nimekuandalia leo kuhusu kampuni ya Samsung, Tuambie unaonaje kuhusu haya..? Je nini ungependa kujua kuhusu Teknolojia tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

5 comments
  1. historia nzuri na nimeifurahia inatufundisha kwamba mafanikio hayaji tu siku moja bali huchukua mda kidogo.. Nilikuwa naomba tufahamishwe simu za sumsung za bei ya chini kabisa na miaka hii na ubora wake.asante

  2. jamani mi naomba mnisaidie nilisikia kuwa simu ya samsung hazichemki yaani hazipati joto wakati unatumia ila me imekuwa tofauti natumi samsung galaxy prime +

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use