in

Samsung Kuja na Toleo Jipya la Samsung Galaxy S9 Mini

Jiandae na simu mpya ya Smsung Galaxy S9 hapo mwakani

Samsung Galaxy S9

Ikiwa bado gumzo lipo kwa watumiaji wa simu za Galaxy S8, Kampuni ya utengenezaji wa simu za Samsung inaendelea kusonga mbele huku ikiwa kwenye hatua za mwishoni kukamilisha simu zake mpya za Samsung Galaxy S9.

Kama tunavyojua utaratibu wa Samsung, simu hizo huzinduliwa mwanzoni kabisa mwa mwaka huku kwa mwaka 2018 tukitegemea simu hizo kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi wa pili, wakati tukiendelea kusubiri ujio wa simu hizo hivi karibuni kumesambaa ripoti za samsung kuja na toleo la tatu la simu za Galaxy S9.

Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes, toleo hilo litakuwa ni simu yenye kioo cha inch 5 na itakuwa ndio toleo la Samsung Galaxy S9 Mini. Tofauti na matoleo ya “Mini” ya miaka iliyopita simu hiyo itakuja na sifa sawa kabisa na simu za kawaida za Galaxy S9 lakini yenyewe itakuwa na utofauti upo kwenye kioo pekee.

Mbali na hayo simu zote za Samsung Galaxy S9 zinatarajiwa kuja na kioo kisicho na ukingo yaani (Infinity Display) Kamera mbili kwa nyumba ambazo sasa zinakuja zikiwa zimetengenezwa kwa teknolojia mpya ya BBAR au ‘broad-band anti-reflection’ hii husaidia kamera kutokuakisi mwanga na mara nyingi hutumiwa na wakongwe wa picha, Najua professional Photographer tunaelewana sana hapa.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Tukiachana na maboresho hayo simu hizo za Galaxy S9 zinasemekana kuja na aina mpya ya processor yenye nguvu zaidi ya SnapDragon 845 chipset, huku pia zikiongezewa na simu zote sasa zitanza kuwa na uwezo wa RAM kuanzia GB 6 tofauti na sasa kwani Galaxy S8 ina anza na RAM ya GB 4 alafu GB 6 kwa Galaxy S8 zinazopatikana kutoka inchini China.

Kwa sasa bado hakuja toka picha kamili yenye muonekano wa simu hizo lakini, mvujishaji wa picha za simu za Samsung anae aminika UniverseIce alivujisha picha hii uku akiandika maneno haya

Tuambie nini maoni yako kuhusu ujio wa simu mpya ya Samsung Galaxy S9..? tuandikie kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment