in

Kutana na Putin-Trump Toleo Jipya Maalumu la Nokia 3310

Toleo Jipya la Nokia 3310 Maalumu baada ya Raisi Putin na Trump Kukutana

Nokia 3310

Hivi karibuni mkutano wa G20 summit umeanza rasmi uko nchini ujerumani mkutano huo ukiwa na lengo la kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu nchi mbalimbali uku ikikutanisha wazungumzaji wa nchi hizo mbalimbali, katika mkutano huu wa mwaka huu raisi trump alikutana na raisi putin wa nchini urusi.

Baada ya kukutana huko kwa maraisi hao wawili, kampuni moja ya Caviar Royal Gift ya huko nchini urusi imetengeneza simu yenye alama ya kukutana kwa maraisi hao. Simu hiyo ambayo ni toleo la Nokia 3310 imetengenezwa kwa kuwekwa chapa za sura za viongozi hao wa urusi na marekani huku ikiwa na imewekewa Titani na muundo wa “Dhamana ya chuma” ambayo ina-elezewa kuwa ni alama ya ulinzi na haki.

Simu hiyo imetangazwa kuanza kuuzwa nchini huku na nchi zingine kwa pesa ya urusi 149,000 Р sawa na dollar za marekani $ 2500 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 5,595,500.00 hiyo ni kwa mujibu wa viwango vya fedha vya siku ya leo. Kwa kawaida simu hiyo ya Nokia 3310 aliyotoka hivi karibuni ambayo ni toleo la kawaida inauzwa kwa gharama ya dollar za marekani $55 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 123,101.00.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Usinunue Simu za Zamani Zenye Umri Zaidi ya Miaka 4

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.