in

PS4 Yaongezewa Uwezo wa Kucheza Game Zake Kupitia Simu

Sasa utaweza kucheza game zako za PS4 kwa kutumia simu yako ya Mkononi

ps4pro

Hii ni kwa wapenzi wote wa game za kifaa maarufu kutoka Sony yaani PS4 au Playstation 4 hivi karibuni wote wataweza kucheza baadhi ya game za kifaa hicho kwa kutumia simu ya mkononi maarufu kama smartphone.

Hayo yametangazwa na kampuni ya Sony kupitia mkutano maarufu wa wapenda game duniani yaani E3 au Electronic Entertainment Expo ambapo sony imesema kuwa sasa italeta huduma ya PlayLink ambayo itakusaidia kubadilisha simu yako ya mkononi kuwa kifaa cha kuchezea baadhi ya game zako za Playstation 4. Moja ya game ambazo zinazo anza kutoka kwa mfumo huo ni game maarufu ya Hidden Agenda Tazama hii..

Ziko game nyingine ambazo zitakuja na uwezo huu baadae mwaka huu lakini ikumbukwe kuwa uwezo huu utakuwa kwa game zile ambazo watu watakuwa wanaweza kucheza zaidi ya wawili yaani kwa lugha ya game ni Multiplayer.

Hata hivyo sehemu hiyo mpya ya PlayLink itakuwezesha kuunganisha simu zenu na kufanya simu zenu wachezaji kuchukua nafasi kama pad ambapo utaweza kufanya mambo mengi ambayo baadhi yake yameonyeshwa kwenye game hii nyingine mpya ya That’s You!

Game hii itakuwa ni moja kati ya game za kwanza ambazo zitakuja na uwezo huo moja kwa moja, game hiyo inategemewa kutoka rasmi mwezi July tarehe 4 na katika kusherekea kuzinduliwa kwa PlayLink game hii itakuwa bure kabisa ili mradi uwe ni mwanachama wa PlayStation Plus. Soma zaidi kuhusu sehemu hiyo kupitia tovuti ya sony hapa.

Kwa habari kamili kuhusu sehemu hiyo lini itatoka na utaipataje au jinsi ya kutumia endelea kutembele Tanzania Tech pia kama unataka habari zaidi za teknolojia unaweza kuendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, kumbuka pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments