in

Tetesi : Picha Iliyovuja ya Simu Mpya ya Samsung Galaxy Note 8

Kama wewe ni mpenzi wa simu kutoka kampuni ya samsung basi soma hii..!

galaxy note 8

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi mbalimbali kuhusu simu mpya ya Galaxy Note 8, lakini hivi leo pia kumezuka tetesi mpya ya picha inayosemekana ndio picha halisi na muonekano wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 8.

Kwenye picha hiyo simu hiyo inayosemekana ndio samsung galaxy note 8 inaonekana kwa nyuma ikiwa na rangi ya Blue Coral lakini inaonekana ikiwa haina finger print kwa nyuma hii ikiwa na maana sehemu hiyo imeamishiwa kwa mbele. Vilevile simu hiyo inaonekana ikiwa na kona ambazo ziko square na wakati kwenye picha nyingine ikiwa inaonekana iko kwa raound.

Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili au uthibitisho kamili kuhusu picha hiyo kama ni ya simu hiyo ya samsung galaxy note 8, lakini kuna uwezekano mkubwa wa picha hiyo kuwa ya simu hiyo inayotarajiwa kutoka baada mwaka huu.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.