Twitter Lite

Twitter Yazindua Twitter Lite Njia Mpya ya Kutumia Twitter

Kampuni maarufu ya Twitter kupitia mtandao wa Twitter hivi leo imetangaza aina mpya ya kutumia mtandao huo huku ikikusaidia kutunza bando lako pamoja na kutumia mtandao huo kwa haraka zaidi, njia hiyo mpya imezinduliwa leo tarehe 6 ili kurahisisha matumizi ya mtandao huo kwa haraka zaidi.

Njia hiyo mpya ambayo ni programu ya mtandaoni kwa sasa ipo hewani na inapatikana kupitia mobile.twitter.com ambapo kwa kutembelea link hiyo utapelekwa kwenye ukurasa ambao ndio utarahisisha matumizi ya mtandao huo uku ukikupa nuwezo wa kutunza bando lako kwa kubofya sehemu ya Data Saver.

Twitter lite pia itakupa uwezo wa kuweka shortcut kwenye kioo chako cha simu huku ikikupa uwezo wa kutumia programu hiyo ya mtandaoni kwa haraka na rahisi. Twitter lite inafanya kazi pia kwa wale wenye simu zenye uwezo mdogo wa internet, jaribu sasa Twitter Lite.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Tovuti
Jinsi ya Kuanzisha Tovuti ya Kisasa kwa Shilingi (Tsh) 3,000 Tu!
Next Post
Sasa Matangazo YouTube ni Kwa Channel Zenye Views 10k Pekee 1

Sasa Matangazo YouTube ni Kwa Channel Zenye Views 10k Pekee