Ifahamu Simu Kutoka Kampuni ya Huawei Honor 8

Mapitio ya simu kutoka kampuni ya huawei
Honor 8 Honor 8

Ni muda sasa umepita toka tuandike mapitio hapa Tanzania tech, kwa mwaka huu kila siku tutakua tunakuletea mapitio ya simu na vifaa mbalmbali kwa njia ya video hii itakupa urahisi wa wewe kujua ubora halisi wa bidhaa hizo.

Basi moja kwa moja twende tukaangalie mapitio ya simu ya Huawei Honor 8, kwa wale wasio jua simu hii ni simu iliyotangazwa huko nchini china na ni simu ya bei nafuu sana ukilinganisha na ubora wake. Muundo na ubora wa simu hii ni wa hali ya juu sana kiasi cha kukidhi haja ya watumiaji wengi wa smartphone hapa Afrika.

Advertisement

Huawei Honor 8 imetengenezwa kwa ubora wa kisasa pamoja na glass maalum ambayo inafanya simu hiyo kuvutia pale unapoiona au unapoishika. Kuhusu ubora wa simu hii….. angalia hapa

Kuelezea kidogo alichokifanya Jerry kwenye video hapo juu ni kuangalia ubora wa simu hiyo ya huawei Honor 8, Jerry alianza kwa kuangali ubora wa kioo kwa kuchukua kifaa maalum na kukwangua kioo cha simu hiyo kwa mpangilio simu nyingi Jerry alizowahi kufanyia jaribio hili mara nyingi huwa zinaanza kuchubuka kuanzia namba tano lakini Honor 8 inaonekana kuwa na kioo bora kidogo na kuchubuka kuanzia namba sita.

Vilevile Jerry alionyesha kuwa simu hiyo imetengenezwa na kuzungushiwa material yenye chuma hivyo kufanya simu hiyo kuwa ngumu kidogo, mwisho Jerry alichofanya ni kuangalia ubora wa simu hiyo kuikunja kabisa, baadhi ya simu alizojaribu zoezi hili nyingi zilikua zikifunjika au kutokufanya kazi kabisa pale zinapokunywa . Kuhitimisha ili kusui uifahamu Honor 8 ni vizuri ujue sifa za simu hii kutoka Huawei.

  • Display 5.2-inch IPS LCD 1920×1080 (423 ppi)
  • Processor HiSilicon Kirin 950 octa-core4xA72 @ 2.3Ghz + 4xA53 @ 1.8Ghz Mali-T880MP4 GPU
  • Storage 32/64GB
  • RAM 4GB LPDDR4
  • OS Android 6.0 with EMUI 4.1
  • Rear cameras Dual 12MP (monochrome + color), f/2.2 1.25-micron pixel equivalent
  • Front camera 8MP, f/2.4
  • Connection USB Type-C (USB 2.0)
  • SIM/MicroSD Dual SIM in Asia
  • Single SIM with microSD (256GB) in Europe/U.S.
  • Battery 3000mAh
  • 9V/2A fast charging
  • Security Fingerprint sensor
  • Other Infrared, bottom mono speaker, VoLTE (T-Mobile only)
  • Waterproofing No
  • LTE Bands LTE FDD: B1/B2/B3/B4/B5/B7/B8/B12/B17/B20
  • Dimensions 145.5 x 71 x 7.5 mm
  • Weight 153 grams
  • Colors Pearl White, Sapphire Blue, Midnight Black

Kuhusu Bei ya simu hii inauzwa kwa dollar za marekani $356.15 wakati kwa hapa tanzania unaweza kuipata simu hiyo kuanzia shilingi za Tanzania TZS 800,000 hadi TZS 920,000.

Je nini maoni yako kuhusu simu hii ya kutoka kampuni ya Huawei Honor 8 tuambie maoni yako hapa chini kwa kuchagua nyota zinazo staili kwa simu hii.

Kwa Mapitio zaidi ya Simu na Vifaa mbalimbali endele kutembele Tanzania Tech kila siku au unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka.

12 comments
  1. Simu hiz nazipenda sana ila chaji ndio shida mm ninayo honor 7i ila chaji da majanga kwanini cm hiz hazikai na chaji???

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use